KIBAKA ALIYECHAPWA NA WANANCHI
Kijana
Mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Omar mkazi wa Mafisa
Morogoro,ambaye ni dereva wa boda boda mwishoni mwa wiki iliyopita
alipokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasir akidaiwa kumpora simu
mwanamke mmoja nayedaiwa kuwa mwanafunzi wa chuo Kikuu Cha Kilimo Cha
Sokoine’ SUA’
Tukio
hilo limetokea ijumaa iliyopita Eneo Mazimbu FK ambapo Mwanafunzi
huyo alikuwa akitembea kuelekea chuoni huku akiongea na simu hivyo Omar
aliyekuwa amempakia mwenzake kwenye pikipiki walimpora simu kwa kutumia
pikipiki hiyo.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Wakihojiwa
na Mwandishi wetu eneo la tukio mashuhuda wa tukio hilo wasliema”huyu
dada alikuwa akieleka SUA huku akiongea na simu ghafla boda boda huyu
aliyekuwa amembeba mwenzake nyuma walimpitia kumpora simu dada huyu na
kukimbia nayo ambapo dada alipiga kelele za mwizi na boda boda wa kijiwe
la FK waliwasha pikipiki zao na kuwafukuza ambapo walifanikiwa
kuwakamata eneo hili la mazimbu reli ya pili ambapo mwenzake aliyempakia
nyuma alifanikiwa kuruka katika pikipiki na kukimbia na kumuachia msara
mwenzake.
Katika
hatua nyingine mmoja wa boda boda aliyefanikisha kukamtwa kwa kibaka
huyo alisema' Hii ni kazi ya boda boda ni kazi kama kazi nyingine na
tunashukuru serikali inatutambua lakini kuna baadhi ya bodaboda
wanatupaka matoke kw akufanya mambo ya wizi huku wakitumia mgongo wa
boda boda ndio maana tulivyoshuhudi tukio hili tumeamu kuteketeza mafuta
yetu na kuwafukuza vibaka hawa na kufanikiwa kuwakamata"alisema Bw
Juma ldd
Mwandishi
wa mtandao huu alipiga simu polisi kwa lengo la kumuogoa mwizi huyu
ambapo fasta Defenda lilifika na kumchukua kibaka huyu ambapo baadhi ya
watu wanaomfahamu walidai anaegesha pikipiki wake kijiwe cha Tumbaku
lringa Road na kwamba pikipiki hiyo alikabidhiwa kwa mkataba wa kwama
mmoja ambapo mwaka ukimaliki pikipiki ni mara yake na kwamba alibakiza
miezi miwili kukamilisha mkataba huo.
Afisa
mmoja wa jeshi la polisi aliyeom,ba hifadhi ya jina lake alimtonya
mwandishi wetu kwamba boda boda huyo alikata roho siku iliyofuata
No comments:
Post a Comment