Watu
saba kati ya 100 Kijiji cha Kenyamanyori, Kata ya Turwa, Wilaya ya
Tarime walioshiriki kunywa dawa ya mganga wa kienyeji aliyeletwa kutoka
Busia nchini Kenya wameingia kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa
kutimiza masharti ya kulipa Sh3 milioni kila mmojaWanakijiji hao
walikusanyika juzi asubuhi baada ya kengele ya kijiji kugongwa na
uongozi, huku wakieleza kwamba ilikuwa siku ya nne kwa kengele hiyo
kugongwa lengo likiwa ni kuzungumzia wizi unaoendeshwa na watu
wasiojulikana.Inadaiwa wizi wa kuvunja maduka umekithiri kijijini hapo,
baada ya wanakijiji hao kuwasili eneo la mikutano, walielezwa kusudio la
kengele kuwa ilikuwa ni kutokana na kukithiri kwa matukio ya uhalifu.
Miongoni mwa waliovunjiwa duka ni Ayubu Wambura, anayedaiwa kuleta
mganga kutoka Busia nchini Kenya kuwabaini wahusika, hivyo kila mmoja
aliombwa kunywa dawa ya mganga huyo au kuacha maana ni hiyari.
Hata hivyo, walitahadharishwa kwamba kama aliyeshiriki hatakunywa dawa hiyo, itamuumbua maana aliyeibiwa atakuwa amekunywa.
Kabla ya kuanza kunyweshwa, mganga huyo aliomba wanakijiji iwapo kuna
mhusika, ni vyema ajitokeze kabla ya kuingia gharama za kuwarejesha
hali yao ya kawaida hazijaongezeka watakaponaswa.
Hata hivyo, wanakijiji walidharau wakidai ni mbabaishaji huyu hawezi lolote kwani hivyo ni vitisho.
Ilipotimu saa 5:00 asubuhi, mganga aliwaeleza ndani ya saa mbili
tangu mtu anywe dawa yake atakuwa ameanza kuonyesha vitendo alivyokuwa
akifanya wakati anaiba dukani.
Saa 6:00 mchana tayari dalili zilikuwa zimenza kuonekana kwa watu
saba wakiwamo wafanyabiashara wenzake, pia yumo mwanamke wakiwa wamelewa
wanafanya vioja, huku wengine wakila nyasi na kutafuna midomo.
Wambura alisema anachotaka ni kurejeshewa Sh12 milioni, zikiwamo
gharama za mganga huyo, huku walionaswa na dawa hiyo wakitakiwa kulipa
Sh3 milioni na kupewa siku tatu vinginevyo watageuzwa vichaa.
“Nimeibiwa sana ila ninavumilia, hii ni mara ya tano sasa, nimechoka
na ninachotaka wanirudishie Sh12.5 milioni gharama niliyotumia ikiwamo
mali zangu walizochukua, waliwahi kunivamia na mke wangu tunatoka dukani
wakatukata mapanga hadi mke wangu akafa,” alisema Wambura.
Pia, tukio hilo lilishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Mji wa Tarime, Vanance Mwamengo, madaktari wa Hospitali ya Mji wa
Tarime, madiwani na polisi na kwamba kutokana na wananchi kutokuchukua
sheria mkononi, masuala hayo yatamalizwa kimila.
No comments:
Post a Comment