Ziba masikio, fanya yako! Wakati
watu wakichonga juu ya sakata la madai ya kuwa na mtoto na utata juu ya
umri wake, Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu anadaiwa kukimbilia
kanisani. Habari
za uhakika zilidai kwamba, baada ya kutwaa taji hilo hivi karibuni na
kuibua sintofahamu, mrembo huyo alikimbilia kwenye Kanisa la Ufunuo kwa
Nabii Yaspi Bendera lilipo Yombo-Buza jijini Dar kwa ajili ya kumshukuru
Mungu kwa kufanikisha ndoto yake ya kuwa Miss Tanzania.
Ilidaiwa
kwamba, Sitti ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Temeke kwa leseni ya CCM,
Abbas Zuberi Mtemvu, akiongozana na mama yake, walikwenda kwenye kanisa
hilo kwa ajili ya kutoa shukrani kwa wema aliomtendea Mungu.
“Watu
wanaendelea kumsema mtoto wa mwenzao huku yeye anamshukuru Mungu kwa
sababu hata kabla hajatwaa taji hilo alikuwa akisali hapa hivyo Mungu
amepokea maombi yake na si vinginevyo kama watu wanavyomsimanga,”
alisema muumini mmoja wa kanisa hilo.
Baada ya kunyetishiwa ishu
hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Nabii Yaspi ili kupata uhakika wa
mrembo huyo kutinga kanisani kwake ambapo alikiri ni kweli alikwenda
kanisani kwake na ameshampigia maombi kwa Mungu hivyo atanyakua Taji la
Miss World mwaka huu.
Sitti
alishiriki shindano hilo tangu ngazi ya vitongoji na kutwaa Taji la
Miss Temeke kabla ya kuibuka kidedea kwenye Miss Tanzania linalofukuta
ambapo kesho (Jumanne), mkurugenzi wa shindano hilo, Hashim Lundenga
anatarajiwa kutoa tamko rasmi.
No comments:
Post a Comment