Tuesday, October 14, 2014

KIJANA AKUTWA AMEFARIKI KORONGONI MKOANI KIGOMA



Mwili ukiwa bado eneo la tukio 
Katika hali ya kustajaabisha kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Yusuph (Me) mkazi wa Buzebazeba Ujiji amekutwa amekufa katika korongo la Lebengera jirani na Ofisi za CCM mkoa katika manispaa ya Kigoma Ujiji huku akiwa amejaa damu katika paji lake la uso
Mara baada ya Jeshi la Polis kufika eneo la tukio walimpekua marehemu na kumkuta na fedha taslimu kama elfu tatu hivi na karatasi ambayo haikujulikana mara moja imeandikwa nini 
tukio hilo limetokea jana Oktoba13 eneo tajwa hapo juu huku umati mkubwa ukiwa umefurika ili kumtambua na kushuhudia tukio hilo, katika uchunguzi wa awali inasemekana tukio hilo limetokea jana usiku kwani kutwa nzima ya jana hapakuonekana mtu ambae amekufa eneo,akiongea na kibonajoro.com mmoja wa wananchi aliekuja kushuhudia tukio,na ambae ni mfanyakazi katika ofc moja jirani na eneo la tukio jina (....) amesema hii imekuwa ni mara ya pili kutokea tukio kama hili la mtu kukutwa ameuwawa na kutupwa katika korongo hili,hivyo tunaviomba vyombo vya usalama kuweka doria ya mara kwa mara eneo hili kwani eneo hili linakaribiana na Bar pamoja na Ofisi za Hazina Ndogo. 
Polisi wakichukua vielelezo katika picha 
Kutokana na eneo alilokutwa marehemu kuwa na miundombinu mibovu ya kumtoa walilazimika kutumia ngazi,hivyo waliomba msaaada wa ngazi kwa gali la emegency la Tanesco na hapa ngazi ilikuwa inashushwa tayari mwili kupandishwa juu kupelekwa eneo husika, 
Mwili ukitolewa tayari kupelekwa kwenye gari la Polisi 
Mwili ukiingizwa kwenye gali la Polis kuelekea Central Polis kwa taratibu zingine 
Mwili wa kijana Yusuph ukiwa ndani ya gari la Polisi,katika taarifa zingine zilizopotikana eneo la tukio zinasema kabla ya kugundulika kwa tukio hili kumetokea tukio lingine linalofanana na hili maeneo ya mwasenga usiku wa kuamkia leo mtu kukutwa ametupwa huku akiwa amepoteza maisha. 
Polisi wakiondoka eneo la tukio 
kwambali ndio eneo la ofisi za CCM mkoa ambapo kulia ndiko kumetokea tukio hili.

No comments:

Post a Comment