Hiki ni miongoni mwa kichwa cha habari zilizopo katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. ni siku chache tuu sasa baada ya watanzania kujiuliza maswali mengi yasiokuwa na majibu sasa serikali yatoa jibu. soma mwenyewe hapo chini
With The permanent secretary in the ministry of foreign affairs and international cooperation Mr. John Haule
From the left side Commissioner of Immigration Hon. Ambokile, SALAAH in the middle and Inspector General of Police Mr. Mangu
with his friend Samuel Sitta on Emirates First Class
Balozi Mdogo wa Tanzania China kwa jina la SALAAAH akiwa na bosi wake Bwana Membe.
Salah akiwa na Balozi Shimbo
With the top Dsm officials from the left next to me The Mayor of DSM Dr. Masaburi, DSM Regional commissioner Mr. Meck Sadick
With my Ninja His excellency Minister of Home Affairs Hon. Chikawe sorting out some issues
Hivi
karibuni kumezuka taarifa za upotoshwaji zilizotolewa kwenye mitandao ya
kijamii kwamba Serikali ya Tanzania imemteua Bw. Salaah, Mkurugenzi wa
Home Shopping Centre, (pichani ) kuwa Konseli wa Heshima (Honorary
Consul) kwenye mji wa Guangzhou kwenye Jimbo la Guandong.
Watoa
taarifa hizo, hawakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yao zaidi ya
kutoa picha mbalimbali za Bw.Salaah kutoka kwenye mitandao mingine ya
kijamii.
Taarifa hizo sio za kweli.
Kwa
mujibu wa Sheria na Kanuni za mahusiano ya kidiplomasia ya China,
nafasi ya Konseli wa Heshima haitambuliki 'mainland' China. Kwa maneno
mengine hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuteua mtu kuwa Konseli wa
Heshima katika eneo lolote la China isipokuwa Hong Kong ambako kuna
mamlaka huru za utawala zinazofuata sheria zake.
Kwa
faida ya umma, ni vema kufafanua kwamba Nchi ya China inakubali nchi za
Nje kufungua Ubalozi kamili (Embassy) ambao makao yake yanatakiwa
kuwepo katika mji Mkuu wa China- Beijing na Konseli Kuu ama kwa lugha
iliyozoeleka Ubalozi Mdogo (General Consulate) ambao unaweza kufunguliwa
kwenye makao Makuu ya mji wowote ule katika Majimbo ya China.
Watu
wengi wamekuwa wakichanganya Ubalozi Mdogo au Konseli Kuu (General
Consulate) na Konseli (Ubalozi) wa Heshima (Honorary Consulate).
Konseli Kuu (General Consulate) ni sehemu ya Ubalozi (ndio maana wengi
huuita Ubalozi Mdogo) ambapo kiongozi wake na maafisa wake wote ni
watumishi wa Serikali kutokea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa. Masharti ya kuwa Mkuu wa Konseli 'General Consulate' lazima
uwe Afisa Mwandamizi wa Mambo ya Nje mwenye uzoefu usiopungua miaka 10
ya Utumishi katika Wizara ya Mambo ya Nje.
Kwa
muktadha huo, taarifa kwamba Bw.Salaah ameteuliwa kuwa Balozi wa
Heshima wa Tanzania huko Guangzhou sio kweli kwasababu Sheria za China
haziruhusu uwepo wa nafasi hiyo. Aidha, Bw Salaah hawezi kuwa Balozi
Mdogo (Consul General) kwa kuwa yeye sio mwajiriwa wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Hivyo habari zinazosambazwa kwenye
mitandao ya kijamii sio za kweli na zinalenga kuupotosha umma.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA MAMBO YA
NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
No comments:
Post a Comment