Thursday, October 30, 2014

TAMKO LA UDSM KUHUSU TETESI ZA KUMTUNUKU DIAMOND PHD YA HESHIMA!




 

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekanusha uvumi kuhusu kumtunuku msanii Diamond Platnumz shahada ya uzamivu (PhD) katika mahafali yake ya 44 yatakayofanyika Mlimani City, Novemba 8 jijini Dar es Salaam.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimekanusha ujumbe uliopo katika mitandao ya kijamii ambao unadai kuwa msanii wa kizazi kipya Naseeb Abdul maarufu kama Diamond atanukiwa Shahada ya Uzamivu ya heshima katika mahafali ya 44 yanayotarajiwa kufanyika Novemba 8 jijini Dar es Salaam.Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimekanusha ujumbe uliopo katika mitandao ya kijamii ambao unadai kuwa msanii wa kizazi kipya Naseeb Abdul maarufu kama Diamond atanukiwa Shahada ya Uzamivu ya heshima katika mahafali ya 44 yanayotarajiwa kufanyika Novemba 8.  

Ujumbe huo ambao ulieleza kuwa Diamond atakabidhiwa shahada hiyo sawa na aliyekuwa mkuu wa chuo hicho marehemu Balozi Fulgence Kazaura katikati mahafali yatakayofanyika katikati ukumbi wa Mlimani City.


Akizungumzia habari hiyo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Yunus Mgaya alisema hakuna kitu kitu kama hicho – ni uzushi usio na ukweli wowote ndani yake

No comments:

Post a Comment