Kuanzia
jana kumekuwa na post kutoka kwa watu tofauti tofauti katika mitandao
ya kijamii kutokana na kifo cha aliyekuwa mwanzilishi wa kanisa la
siloam nabii Eliya. moja ya post ni hapo chini. Kuna habari zinaenea kwa
kasi katika mitando ya kijamii ya kwamba ,mwenye mafundisho tata
,Ndungu Munuo,aka Adamu wa Pili, Nabii Eliya, Bwana wa Majeshi, Mjumbe
wa Mapenzi ya Mungu wa Kizazi cha Nne, Amefariki Dunia jana usiku, Mpaka
sasa hakuna tangazo rasmi la Kanisa la Siloam. Sitofahamu hiyo
inatokana na kutokuwa na taarifa za uwazi za kifo chake. kutokana na
sintofahamu hiyo blog hii ilifanya mawasiliano na mmoja wa washirika
wake kutaka kujua uharisia wa jambo hilo Kwa mujibu ya Mshirika
niliyeongea nae amesema kuwa nabii Elia amelala na wala hajafa
na hakuna kulia maana aliwaaga watu wote wakiwamo ndugu zake na familia
yote na jambo hili lilikuwa linajulikana kuwa atalala na alishatafuta
hadi mrithi wake ambaye ataendeleza kazi. anategemewa kulazwa mlima wa
moto
(nyumbani kwake) mbezi bichi siku ya tano ya umbaji ambayo ni j2.
aliongeza kusema kuwa muda wa yeye kutumika wa miaka 3 ulishaisha hivyo
alishamaliza kazi. alinipa mifano kuwa manabii wengi walifanya kazi kwa
miaka 3 na wakawa wamemaliza kazi yao hivyo na nabii Elia kuanzia
ameanza kazi miaka 3 ilishafika ni lazima aondoke ili wengine waendelee.
Mshirika huyo alikuwa anaongea kwa ujasiri na kujiamini kana kwamba
alishafundishwa namna ya kujibu, kutokana na mahojiano niliyofanya nae
ni kweli Nabii Eliya kafariki na maandalizi ya kumlaza nyumbani kwake
zinaendelea haijafahamika kama alikuwa anaumwa au alifariki ghafla.
Aliyekuwa Nabii Eliya wa kanisa la siloam shika neno trnda neno Nabii
Eliya akiwa madhabahuni Wafuasi wakijipanga wakati wa yeye kuingia Kwa
heri nabii Eliya
No comments:
Post a Comment