Thursday, August 28, 2014

HALIMA MDEE AMWAGA MACHOZI HADHARANI BAADA YA KUPEWA FOMU YA KUWANIA UENYEKITI WA BAVICHA



Vigogo wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), watachuana katika kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa baraza hilo baada ya jana baadhi ya wanawake kujitokeza kumchukulia fomu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.Mbunge huyo anaungana na Mbunge wa Viti Maalumu, Chiku Abwao na wanachama wengine, Lilian Wasira na Sophia Mwakagenda ambao nao wamesharejesha fomu kuwania nafasi hiyo inayoshikiliwa na Suzan Lyimo.Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Agosti 30 na uchaguzi unatarajiwa kufanyika Septemba 11, mwaka huu.
Wanawake zaidi ya 30 kutoka Kinondoni, Kawe, Pwani na Ubungo jana saa 5.20 asubuhi, walifika katika ofisi za Bawacha jijini Dar es Salaam kumchukulia fomu Mdee wanayedai kuwa ndiye anayestahiki kuliongoza baraza hilo kutokana na msimamo wake wa uongozi wa kutotaka kuyumbishwa.

“Tumekaa na kutafakari ili kumpata mwanamke atakayeweza kuliongoza baraza hili kwa kututoa hapa tulipo na kutupeleka mbele zaidi, tumeona Halima Mdee anatufaa zaidi ndiyo maana tumeamua kuja kumchukulia fomu,” alisema Felister Njau, Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kawe.
Huku akishangiliwa na wenzake alisema, “Tunakwenda kumtafuta sehemu yoyote alipo ili tukamkabidhi hii fomu na tutamwomba akubali ombi letu.”
Msafara wa wanawake hao wakiwa na fomu yao mkononi ukiongozwa na Mwenyekiti wa Wazee Kata ya Kunduchi, Elefedina Mali ulikwenda makao makuu ya chama hicho ambako walimkuta Mdee na kumkabidhi fomu hiyo.
Aliwashukuru na kuwaomba wamvumilie kwani anahitaji muda wa kulitafakari ombi hilo.

Huku akibubujikwa na machozi, Mdee (pichani) alisema; “Nimewaelewa naombeni nikajitafakari kwanza, nitawaeleza nitakachoamua.” Wanawake hao pia walichangishana fedha Sh53,000 walizomkabidhi Mdee kwa ajili ya kurejeshea fomu hiyo.

MADAKTARI WANASWA WAKIMTOA MIMBA MWANAFUNZI

 
Madaktari wawili, Hamis Chacha (kushoto) na Shengena wanaotuhumiwa kwa jaribio la utoaji mimba.
 

IMEBUMA kwao! Madaktari wawili, Hamis Chacha na Shengena wa zahanati moja iliyopo Yombo Buza jijini Dar wamejikuta katika wakati mgumu baada ya polisi kuwaibukia na kuwaweka chini ya ulinzi kwa madai ya  kufanya jaribio la kumchoropoa mimba msichana mmoja aliyedaiwa kuwa ni denti wa chuo f’lani cha digrii za juu, Dar.

Tukio hilo la aina yake lilijiri Agostii 25, mwaka huukatika zahanati hiyo ambayo jina tunalihifadhi kwa sasa.Awali, Operesheni Fichua Maovu  ‘OFM’ ya Global Publishers  ikiwa katika pitapita zake ilinasa tukio hilo ambapo polisi walikuwa ndani ya zahanati hiyo wakiwaweka chini ya ulinzi madaktari hao.
OFM ilifanikiwa kuzama ndani ya zahanati hiyo na kuingia kwenye chumba cha kilichodaiwa hutumika katika zoezi hilo.
 
Vifaa vilivyokusudiwa kutumiwa na madakta hao katika zoezi la utoaji wa mimba.
 
Daktari Shengena alipoona kamera ya OFM alitaka kukimbia licha ya kuwepo kwa askari ndani ambapo walitumia nguvu za ziada kuwadhibiti vyema na kuingizwa ndani ya chumba alichokuwemo mwenzake ambaye naye alinaswa akiwa na vifaa vilivyodaiwa ni vya kuchomolea mimba akiwa amevificha kwenye mfuko wa rambo.
 
Madaktari wakiwa chini ya ulinzi wa makamanda wa OFM.
 
Baada ya maafande kuwaweka chini ya ulinzi, madaktari hao walizua kituko kufuatia kuzitupa chini shilingi 40,000 walizopewa na denti huyo kama malipo ya kazi hiyo wakidhani ni za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘Takukuru’.
 
kiasi cha fedha cha Shillingi arobaini elfu walicholipwa madaktari kwa ajili ya kufanikisha zoezi la utoji mimba.
 
Wakizungumza na waandishi wetu baada ya kuulizwa nini kilikuwa kikiendelea chumbani humo, Dokta Chacha alidai kuwa mgonjwa huyo ana tatizo kwenye kizazi hivyo alikuwa akitaka kusafishwa na si kutoa mimba maelezo yalikosolewa na denti huyo aliyedai kuwa alikwendwa kwa mapatano ya kumchoma mimba ili akaendelee na masomo chuoni.
 
Binti (denti) aliyekusudiwa kutolewa mimba.
 Akijibu kuhusu kwa nini alivificha vifaa va kutolea mimba kwenye mfuko, Dokta Chacha alijiumauma na kusema denti huyo alifuata taratibu zote kama wagonjwa wengine, lakini alishindwa kuonesha risiti au cheti cha kumsajili mgonjwa huyo kwa ajili ya matibabu.
 
Zahanati iliyotumiwa na madaktari hao katika jaribio la utoaji mimba.
 Kichekesho kingine kilikuwa wakati OFM na wanausalama wakitoka nje ya zahanati hiyo na watuhumiwa na kukuta kwenye maeneo mengine kukiwa kweupe na kusemekana kuwa, madaktari na manesi walioshuhudia wenzao wakitaitiwa walitoka nduki kwa kuogopa ushahidi.

Mwishowe watuhumiwa hao walifikishwa katika Kituo cha Kidogo cha Polisi Buza na kufunguliwa jalada lenye Kumbukumbu Na. BUZ/RB/32/2014 kabla ya baadaye kufikishwa Kituo cha Polisi Chang’ombe, Dar kwa ajili ya mahojiano ya kina kuhusiana na sakata hilo.

BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LIMEFUNGULIWA JANA JIJINI DAR ES SALAAM


1Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) la kwanza kufanyika Dar es Salaam, tangu utaratibu wa kufanyika kwa bunge hilo kwa mzunguko kwa kila nchi mwanachama wa Jumuiya.
2Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo.
3Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda (kushoto) akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa wakati wa ufunguzi wa vikao vya bunge hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo4Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Abdullah Juma Saadala (wa pili kushoto), akifuatilia ufunguzi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Phyllis Kandie  (Waziri kutoka Kenya) Shem Bagaine (Waziri kutoka Uganda), Leontine Nzeyimana (Waziri kutoka Burundi), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Jumuiya hiyo Wilbert Kaahwa6Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Jumaa Saadala akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam7Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia hutuba ya Spika wa bunge hilo (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

KIJANA APIGWA HADI KUFA BAADA YA KUIBA SIMU MBEYA



Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Mwakilalo (25) mkazi wa Block T alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mbeya baada ya kupigwa na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi kwa tuhuma za kuiba simu.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 02:15 usiku huko katika maeneo ya Block T, jiji na mkoa wa Mbeya. Inadaiwa kuwa marehemu alikamatwa na kuanza kupigwa na wananchi hao na badae alipelekwa na kufungiwa katika ofisi za mtendaji ambapo alitoroka na ndipo wananchi hao walimuona na kumkimbiza na kuanza kumpiga hali iliyopelekea kumvunja mkono wake wa kushoto na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya. Juhudi za kuwatafuta waliohusika katika tukio hilo zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wawafikishe watuhumiwa wanaowakamata kwa makosa/tuhuma mbalimbali katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria.

CHINA YAUNGANA NA TANZANIA KUTOKOMEZA UHALIFU


pic no 1
Na. Tamimu Adam – Jeshi la Polisi
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imekabidhiwa msaada wa vifaa vyenye thamani zaidi ya milioni mia moja kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa ajili ya matumzi ya ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya ndani na ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Polisi Tanzania.Msaada huo, ulitokana na Ziara ya Naibu Waziri wa Usalama wa raia wa Jamhuri ya watu China aliyoifanya hapa nchini mwezi mei mwaka jana ambapo aliahidi misaada mbalimbali kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Polisi.Miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa na Balozi wa Jamhuri ya watu wa China hapa nchini Mhe. Xu Youqing kwa Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Pereira Silima ni pamoja na Kompyuta Thelasini (30), Viti tisini na mbili (92), Meza hamsini (50) na PA System kwa ajili ya kumbi mbili za mikutano.

Aidha, Balozi wa Jamhuri ya watu wa China hapa nchini Mhe. Xu Youqing alikabidhi Pikipiki hamsini (50)   kwa Jeshi la Polisi ambazo zilipokelewa rasmi na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima. Pikipiki hizo zilitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya watu wa China kwa niaba ya jumuiya ya wafanyabiashara wa kichina walipo Afrika wakati wa ziara yake aliyoifanya hapa nchini mwezi juni mwaka huu.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Pereira Silima baada ya kupokea vifaa hivyo, alimshukuru Balozi huyo wa China na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Pamoja na Wafanyabiashara wa Kichina waliopo Afrika kwa msaada walioutoa kwa Serikali ya Tanzania, na kueleza kuwa vifaa hivyo vyote vitakuwa ni chachu katika kuzuia, kupambana na kukabiliana na uhalifu hapa nchini.
Naye, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki alisema kuwa mbinu za kutenda uhalifu hubadilika mara kwa mara kulingana na mabadiliko ya kiteknolojia, na katika kukabiliana na mabadiliko hayo Jeshi la Polisi liko kwenye utekelezaji wa Maboresho yaliyojikita katika mihimili mikuu mitatu ambayo ni kulifanya Jeshi kuwa kisasa, lenye weledi na linaloshirikiana na wananchi katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu, hivyo vifaa vilivyokabidhiwa vitalisaidia Jeshi la Polisi katika mpango huo unaolenga kuzuia uhalifu.

ZITTO KABWE AONGELEA UHUSIANO WAKE NA DIVA LOVENESS


KWA mara ya kwanza Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe ameibuka na kuzungumzia uhusiano wake na mtangazaji wa Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ na kufuta uvumi mzito uliokuwa ukizagaa kuwa wawili hao ni wapenzi.

Zitto alifunguka hayo juzi kupitia kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Televesheni ya East Africa ambapo alikanusha kuwa hana uhusiano wowote wa mapenzi licha ya kudaiwa kutungiwa wimbo na mtangazaji huyo kama ishara ya penzi lao.“Mh! Kama yeye amenitungia wimbo sijui lakini mimi sina uhusiano naye wowote wa kimapenzi,” alisema Zitto.

Katika mahojiano hayo, mheshimiwa huyo alifungukia skendo nyingine inayomhusisha kutembea na staa wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi na kudai hakuna ukweli wowote juu ya ishu hiyo.

Alisema anaumia zaidi kusikia watu wanavyomhusisha kutembea na Mwasiti kupitia mitandao ya kijamii wakati hakuna ukweli wowote ambapo msanii huyo wanaheshimiana na kufanya naye kazi kwa karibu ili kumsaidia katika harakati zake za muziki.

“Naumia sana kusikia wakinisema na Mwasiti wakati yule ni dada yangu na mbaya zaidi ni mtu ambaye mara kwa mara nimekuwa nikimsaidia katika shughuli zake za muziki, hakuna kitu kingine zaidi ya ukaka na udada,” alisema Zitto.

Aidha, mheshimiwa huyo mbali na kungumzia mikakati yake ya kisiasa katika kipindi hicho, aliweka bayana kuwa ni baba wa mtoto mmoja kwa mkewe aliyemtaja kwa jina moja la Jack, wanamlea mtoto wao vizuri lakini suala la ndoa bado halijatimia.

Wednesday, August 27, 2014

OLIVER MTUKUZI AONYESHA MATOKEO YA VIPIMO VYAKE VYA UKIMWI HADHARANI


Mwanamziki mkongwe Oliver Mtukudzi, ameonyesha hadharani matokeo ya vipimo vyake vya ugonjwa wa ukimwi baada ya kuwepo kwa maneno maneno mtaani kwamba mwanamziki huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 60 kuwa mgonjwa wa ugonjwa huo hatari.

Hata hivyo katika majibu ya vipimo hivyo mwanamziki huyo alionekana kutokuwa na ugonjwa huo, alikiri kuwa ndugu zake wengi wamefariki kwa ugonjwa huo, lakini yeye anasumburiwa na ugonjwa wa kisukari na sio mwathirika wa Ukimwi.