Tuesday, September 30, 2014

NABII ALITIKISA KANISA KWA KUFANYA MIUJIZA...MAELFU WAMIMINIKA KANISANI KWAKE


Na Mwandishi Wetu
Nabii wa Kanisa la Holly Ghost Fire lililopo Mbezi Juu – Kwa Temba ameendelea kuwa gumzo jijini Dar kwa miujizo anayoitenda kwa kuwaombea wagonjwa ambao wanapona Live bila King’amuzi.
Vyombo mbalimbali vya habari ukiwemo mtandao huu vilishuhudia maajabu ya nabii huyo anaejulikana kwa jina Jeremiah Lukiko “ Mzee wa Fire” vilishuhudia muujiza miujiza mbalimbali ya kuwaponya watu wenye ukoma pamoja magonjwa sugu yote.
Kanisa hilo ambalo licha ya kuwa change lakini maelfu yaw a waumini wamekuwa wakimiminika kwa ajili ya kupata huduma bora ya maombi yaliyojaa upako wa ajabu toka kwa mtumishi huyo wa Mungu natayari watu wengi wameanza kuhama makanisa mengi na kukimbia kwake kwa ajili ya kuponywa magonjwa yao.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ibada kumaliza mwishoni mwa juma Mchungaji huyo alisema” Hii ni miujiza ya kutisha Mungu anatenda kazi yake hapa hatuna mzaha na suala la uponyaji hapa hata ukija mgonjwa umebebwa kwenye machera haraka tu moto unafanya kazi yake hivyo natoa uwito kwa watanzania sasa waache kuteseka Mungu amewaleta mkombozi hata kama wamehangauika namna gani na magonjwa lakini hapa kwangu ni mwisho waje na Mungu atawaponya kwa maombi yangu na kwa uharaka zaidi” Alisema Nabii Jarry









Mtumishi huyo alitoa uwito kwa wakazi wa Jiji la Dar na vitongoji vyake kuacha kuteseka na maradhi, au wasiogope nguvu za kichawi, au chuma ulete na wale wenye umaskini wa kurithi pamoja na laana ya kurithi wafike Kanisani kwake awashughulike kwake ni kazi ndogo hiyo maombi pekee yanaweza kubadilisha maisha ya mtu kwa dakika kadhaa.


Na ratiba zinaanza kila siku za Jumatano, Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi, ni saa kumi jino na Jumapili ibada inaanza saa tatu asubuhi hasi saa saba mchana na kwa wale wenye mahitaji ya maombi wapige namba ya huduma 0713-976786




































ANGALIA PICHA MICHEZO HATARI DUNIANI WALA USIJARIBU


Hii ishara inaonesha kuwa hautakiwi kunywa pombe .. sasa huyu jamaa anapata shida sana akitaka kunywa maji au chakula maana anatafuta kanafasi kadogo ili kufanya hivyo.
Ni alama ya tahadhali hii ni moja ya mamia ya watu ambao hawali nyama huko Thailand , huyu anaamini kwa kujiweka mapaga makali na kujichoma hivi itasaidia watu kuacha maovu kabisa na kuwapa amani mioyoni mwao
Hii ni hali ya kawaida sana kwao 
Huu ni utalii kabisa ambapo watu wengi wanaenda kuutazama , ikiwa kama kwetu pia likitokea kundi kama hili wanaokataa mambo maovu kwa mtindo huu itakuwa ni sehemu nzuri ya utalii
Hebu mtazame kwa umakini huyu jamaa yeye amejichoma na sindano kibao hapa chukua muda wako uzihesabu
Huyu kasha kula sana vyuma
Hii ni sema hapana kuto kula nyama, kufanya mapenzi na kunywa pombe 
Hii inamaanisha ni lazima kuangamiza maovu 
Haya si mapambo lakini hawa wanakataa matendo ya ajabu ajabu 
Sasa huyu ametobolewa na kuwekwa makamba mdomo mzima pia wanapigania kuacha na kutokomeza uhalifu 
Hapa Jibu unalo
Hapa wanaaminini nkabisa kwa kufanya hivi wanasema hapana kabisa uhalifu kataa uhalifu ndio maana yake hapa
Sasa Tazama huu Mjambia hapa jamaa analamba hajali vipi anaumia lakini anamaanisha uhalifu basi 
Tazama nanasi hizo zimepita katika waya ambao unasaidiwa na midomo yao ambauyo wamechomwa 
mambo yanaendelea 
Hapaana mchezo
MAELEZO NA THIS DAY MAGAZINE PICHA NA GATTY IMAGES/AFP/REUTERS

MGOGORO WA KIMAPENZI WASABABISHA MUME KUJINYONGA

FUNDI AJINYONGA

Emmanuel Carlos enzi za uhai wake. Habari kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, kwa muda mrefu, marehemu alikuwa na mgogoro usioisha na mkewe Mariamu Suleimani uliosababisha wawili hao kulala katika vyumba tofauti ndani ya nyumba yao. Baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema kutokana na ugomvi huo, marehemu alikuwa akirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na kumtukana matusi mkewe huku baadhi wakienda mbali na kudai alikuwa haachi hela ya matumizi. 
hali ya kushangaza, mtu mmoja ambaye ni fundi seremala aitwaye Emmanuel Carlos, mkazi wa Kwabinyau Magomeni jijini Dar amekutwa akiwa amejinyonga saa mbili asubuhi Septemba 23, mwaka huu katika kile kinachodaiwa kuchoshwa na mgogoro wa kifamilia.
Hata hivyo, mkewe marehemu anadaiwa kuwa na biashara yake ya samaki na alikuwa akijituma ili kuhakikisha anapata nauli ili arejee nyumbani kwao. 
Mke wa marehehu akilia kwa uzuni. Kwa mujibu wa maelezo yaliyopatikana, mtu wa kwanza kujua kuhusu suala hilo alikuwa ni kijana wake mwenye umri wa miaka saba, Celestine Carlos aliyekwenda chumbani kwa baba yake kuomba hela ya shule, ambapo alimkuta akining’inia kwenye dari baada ya kuwa amejifunga kamba kwenye feni. 
Akizungumza na waandishi wetu Mariamu alisema kuwa siku moja kabla ya tukio, mumewe alirudi nyumbani na kumtukana huku akilia na kumwambia kuwa atamkumbuka sana katika maisha yake na kwamba kabla ya kupambazuka mmoja wao atakuwa amekufa. 
“Siku iliyofuata alipoamka alinikuta naosha vyombo, akanitazama kwa jicho baya kisha akaenda chumbani kwake ambako alijifungia.
Baadhi ya wananchi wakiwa eneo la tukio. Nusu saa baadaye alikuja mwanaye Celestine na kuniomba hela ya shule, nikamwambia aende akachukue kwa baba yake, alipoingia akarudi na kuniambia baba yake ananing’inia, jambo nililoona kama utani lakini baadaye nilienda na kumkuta akiwa amejinyonga,” alisema Mariamu huku akilia kwa uchungu. 
Naye mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Jumanne Mneka alikiri kufahamu mgogoro wa familia hiyo na kusema walikuwa wakiwasuluhisha kila mara. 
Polisi wakiwa eneo la tukio. “Juzi kati tu tumetoka kuwapatanisha, nashangaa leo saa mbili asubuhi napokea taarifa kuwa Emmanuel amejinyonga, nimehuzunika sana,” alisema. 
Majirani wakiwa wameshtushwa na kushangazwa na jambo hilo, waliungana na wapita njia kwenda kushuhudia tukio hilo, hali iliyoufanya mtaa huo usipitike kwa muda.
Waandishi wetu waliwashuhudia polisi wakifika eneo hilo na kuuchukua mwili na kuupeleka katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi. Marehemu ameacha mke na watoto wawili.

CHADEMA, UKAWA WAANDAMANA DAR

Wananchi wamefanya maandamano huko Manzese jijini Dar es Salaam wakipinga kile wanachokiita ni wizi unaoendelea ndani ya bunge Maalum la Katiba ikiwa ni mwendelezo wakutimiza tamko la Mwenyekiti wa CHADEMA na UKAWA la kufanya maandamano nchi nzima kupinga mchakato huo.

ANUSURIKA KUUAWA KWA KUCHOMWA MOTO AKIDHANIWA NI MWIZI

 MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard Osward (40) mkazi wa Tabata Segerea, hivi karibuni alinusurika kuuawa kwa kuchomwa moto na wananchi baada ya kuhisiwa kuwa mwizi alipokutwa alfajiri akiwa na mfuko ambao ndani yake kulikuwa na bomba, huko Segerea.

Richard Osward aliyechomwa moto na watu wenye hasira kali akidhaniwa kuwa ni mwizi. Akizungumza kwa shida akiwa katika wodi namba 23 iliyomo ndani ya Jengo la Sewa Haji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Richard alisema tukio hilo lilimkuta akiwa ameongozana na rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Moses na kwamba walikuwa wakielekea Gerezani, Kariakoo ambako wanajishughulisha na ufundi wa magari.



Akiuguza majeraha ya moto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. “Nilitoka nyumbani nikiwa nimebeba bomba katika mfuko nikitaka kwenda kuliuza, tulipofika Segerea Seminari, tulisimamishwa na watu ambao walitutilia shaka wakaanza kutupekua. 
“Wakasema sisi ni wezi na hivyo lazima watuadhibu. Mara akapita dereva wa bodaboda ambaye alishinikiza kuwa sisi ni wezi na kutaka wachange hela wakanunue petroli ili watuchome moto, uzuri ni kwamba kwa kuwa ilikuwa usiku,wakashindwa kupata hayo mafuta,
lakini tunashukuru dada mmoja alikuja amevaa sare za kampuni moja ya ulinzi, akatukingia kifua na kusema watupeleke polisi na ndiyo tukafikishwa Kituo cha Polisi cha Stakishari na baadaye kunileta hapa kwa matibabu, kilichoniponza ni njaa lakini mimi ni mtu safi katika jamii, mwenzangu alifanikiwa kukimbia.”