Thursday, September 18, 2014

DIAMOND AWAFUNGUKIA WADADA


Diamond platnumz katika ururasa wake wa facebook amepost post ambayo ina mashiko sana kwa madada wa kibongo wanaojiona wao wako juu sana wanaona wakiza watapoteza mvuto kwa watu diamond akaamua kufunguka kiivi.Kwa mtazamo wangu mimi naona kuzaa hakumfanyi mtu azeeke au awe wa kizamani, ni tabia tu ya mtu mwenyewe.... na ndiomaana dada zetu kama Beyonce, Nancy sumary, Kim Kardashian na kadharika wana watoto na still wanafanya vizuri.....Au we mtazamo wako ukoje?
(I believe, bearing kid (s) doesn't transform a woman being old or being out of fashion.....it's her natural Behavior...my living proof are, Beyoncé, Nancy Sumary, Kim kardashan etc.... Isn't it??? Let me hear your views on this....)

MAMA AFUNGUKA MAAJABU ANAYOYAFANYA MWANAE NA KUSEMA NI MAZITO NA YANATISHA

Mtoto Happiness (10) anayedaiwa kuzua kizazaa mjini Zanzibar.

MTOTO Happiness (10) (pichani) ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita  alizua kizazaa mjini Zanzibar baada ya kuonekana akizungumza na viumbe wa ajabu na wanyama, ametua jijini Dar kufuatia kufika kisiwani humo kimaajabu.Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Sarah Zefania, mwanaye Happiness alianza kuonesha maajabu Zenji tangu alipoonekana kwenye uwanja wa ndege kisiwani humo wiki iliyopita.
Alisema maofisa wa uwanja huo walipigwa butwaa baada ya kumwona mtoto huyo uwanjani amepita sehemu zote za ukaguzi ambazo abiria asiyekaguliwa nyaraka zake za kusafiria na mitambo maalum ya kuangalia vitu mbalimbali vikiwemo kemikali hatari, silaha na madawa ya kulevya hawezi kupita.
Kwa mujibu wa mama huyo, aliambiwa na maofisa wa uwanja huo kuwa sehemu hizo zote mtoto wake alipita bila kuonekana na kamera za uwanjani hapo wala kuacha kumbukumbu yoyote hali iliyozidi kuwaumiza vichwa maofisa wa uwanja huo.
Zefania alisema wakati maofisa hao wakitafakari hayo, ndipo msamaria mwema mmoja alijitokeza na kumchukua kwenda kumuhifadhi nyumbani kwake.Mtoto Happiness akiwa na mama yake mzazi, Sarah Zefania.

“Akiwa nyumbani kwa msamaria mwema huyo, nimeambiwa mwanangu alianza kumfanyia maajabu mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wanyama na viumbe wengine wa ajabu au kutoka nje huku mlango umefungwa kwa ndani.
“Kuna muda alizungumza na viumbe wasioonekana ambapo aliwasiliana nao na kumletea vitu kadhaa alivyovitaka. Wakati mwingine alizungumza na wanyama wa mle ndani, kama kuku na paka ambao alikuwa akiwatuma kumfanyia yote aliyokuwa akiwaagiza.
“Hali hiyo ilimshtua yule msamaria mwema naye aliomba kupambazuke ili ampeleke mwanangu ustawi wa jamii. Yaani nahisi pengine angekuwa amemuokota sehemu bila kukabidhiwa mbele ya mashahidi pengine angemtupa usiku huohuo.
“Baada ya kushuhudia vituko hivyo, asubuhi iliyofuata alimkimbiza ustawi wa jamii ambako nako wameniambia alianza kuwafanyia vituko kama hivyo na kuwaambia kuwa angewatoroka muda wowote, kisha kuonekana akiparamia juu ya paa na kutaka kutoka.
“Yaani kwa muda mfupi waliokaa naye, maofisa wa ustawi wa jamii wanasema amewahenyesha vya kutosha ndipo walipofanya juhudi za kunitafuta na mimi nikaenda kumfuata,” alisema mama huyo muda mfupi baada ya kutua bandarini Dar.

Mtoto Happiness katika pozi.

Paparazi wetu alipomtaka mtoto huyo kuzungumza alikataa katakata na kujifanya bubu hali iliyomshangaza hata mama yake. “Nashangaa, sijui kwa nini hataki kuzungumza na wewe wakati ni mzungumzaji sana,” alisema mama Happiness.
Akizungumzia historia ya mtoto huyo, mama huyo alisema alimzalia Musoma, Mara na mwanaume mmoja aliyemtaja kwa jina la Juli ambaye walitengana na hawana mawasilino mazuri.
Mama huyo alisema alimpeleka mtoto wake shuleni lakini kila akifika harudi nyumbani na kutorokea anakokujua na kuonekana baada ya wiki mbili au tatu.
Kufuatia hali hiyo amewaomba wasamaria wema na viongozi wa dini kumwombea mtoto wake ili arudi katika hali ya kawaida kwani anajua kuna mkono wa mtu wa karibu uliyemharibu mtoto wake.

Wednesday, September 17, 2014

MKUU WA KITUO CHA POLISI NUSULA AUAWE NA WANANCHI BAADA YA KUFUMWA AKITAKA KUMBAKA MWANAFUNZI


Mkuu wa kituo cha polisi cha Nyamboge kilichopo katika kata ya Katoma wilayani Geita mkoani Geita amenusurika kuuawa na wananchi wenye  hasira kali  baada ya kukutwa akitaka kufanya mapenzi na mwanafunzi katika chumba anachoishi mwanafunzi huyo(Geto).

Tukio hilo limetokea juzi  Jumapili  majira ya saa tatu usiku ambapo wananchi wakiwa na marungu na mikuki waliweka mtego wa kumnasa mkuu huyo mwenye namba E 2837 Koplo Venance.

Akielezea tukio hilo binti huyo (jina linahifadhiwa)(19) anayesoma kidato cha nne alisema siku ya jumapili mkuu huyo wa kituo alituma maaskari wawili wiki jana wakaenda kumkamata.

"Hata sijui kosa langu,nilikamatwa nikalazimika kwenda na nilipofika alianza kunilazimisha natembea na mwalimu wangu,nilipokataa nilianza kupigwa na kulazimishwa kuandika maelezo",alisema mwanafunzi huyo.

Alisema baada ya kukataa kuandika maelezo alipelekwa rokapu na muda mfupi baadaye  alifuatwa na askari mmoja kati ya wale waliomfuata anapoishi, alianza kuandika maelezo na kumlazimisha kusaini.

Alisema  baada ya kugoma kuandika alipigwa sana na kuamua kusaini kutokana na kutishiwa kufungwa na baada ya kusaini aliitwa na OCS huyo na kumwambia aende nyumbani lakini arudi jioni ana shida naye ya muhimu sana lakini hakurudi kutokana na kuchoka na kipigo alichokipata kituoni hapo.

"Kutokana na mkuu huyo wa kituo kutuhumiwa na mwanafunzi kuwa anamtaka kimapenzi ilibidi awaambie wanafunzi wenzake na wananchi na baada ya hapo wakatengeneza mtego ili wamnase",walisema mashuhuda wa tukio hilo.

"Siku ya jumapili  mkuu huyo wa kituo alikwenda nyumbani kwa mwanafunzi huyo na kuomba wafanye mapenzi kwa kuwa wenzake anaoishi nao hawakuwepo lakini aligoma kufanya hiyo ",walisema mashuhuda wa tukio hilo  na  kuongeza:

"Kutokana na mtego wa wananzengo,muda mfupi   wananchi waliokuwa wamemuona OCS anakwenda kwa binti huyo walifika hapo na kufunga mlango kwa nje na kuanza kupiga mwano".
 

UKATILI DHIDI YA BINADAMU UNAOENDELEA NCHINI IRAQ NI HATARI


Hakika   binadamu   tumekuwa  kama  wanyama,   Angalia  mauaji  yanayofanywa  na  waasi  huko  iraq  hakika   yanatisha   sana
 






Huyu  ni  mwanajeshi  wa  serikali  ambaye  aliuwawa  na  waasi  wa   iraq
Hawa  ni   wanajehi   wa   Iraq  ambayo  waliuwawa  na   kikundi  cha  waasi  huko  iraq

Tuesday, September 16, 2014

REGINALD MENGI AINGIA FAINALI TUZO YA MFANYABIASHARA BORA AFRIKA

 

MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi ni miongoni mwa wafanyabiashara wanne waliofikia fainali ya kuwania Tuzo ya Mwaka ya Mfanyabiashara Bora Afrika (AABLA), kundi la Afrika Mashariki.


Sherehe za tuzo za AABLA, kundi la Afrika Mashariki zitafanyika Septemba 20 mjini Nairobi, Kenya na zitarushwa hewani na runinga barani Afrika.
Kwa mujibu wa chaneli ya runinga ya masuala ya fedha na biashara Afrika (CNBC Africa), ambao ndio waandaji wa sherehe hizo, tuzo hizo za kila mwaka zimebuniwa kwa ajili ya kutambua utendaji uliyotukuka katika biashara, wenye mafanikio makubwa kwenye sekta zao za biashara na vile vile kwenye jamii ambako biashara hizo zinaendeshwa.
“Tuzo hizo ni kutambua uongozi wa watu hao katika kubadilisha sekta ya biashara kwa kuendeleza ubora wa shughuli zao kwa kuzingatia desturi njema za kufanyabiashara na ubunifu,”.
“CNBC Africa, inajivunia kuendeleza utamaduni uliowekwa na tuzo hizi unaotambua na kusherekea mtazamo, msukumo wa mafanikio na ubora mkubwa wa viongozi wafanyabiashara katika bara la Afrika. AABLA inawatambua kipekee na kuwaheshimu viongozi ambao wamechangia katika kuboresha uchumi wa Afrika na waelekezi wa biashara zinazoongoza sasa,” ilisema taarifa hiyo kupitia tovuti : http://www.aabla2014.com.
Wafanyabiashara wengine watatu wateule wa tuzo hiyo ni Ofisa Mtendaji wa Britam, Benson Wairegi, Ofisa Mtendaji wa Centum, James Mworia, na Ofisa Mtendaji wa Crown Paints, Rakesh Rao (Kenya).
Watanzania wengine waliyoteuliwa katika tuzo hizo kwa makundi tofauti ni Ofisa Mtendaji wa Helvetic Solar Ltd, Patrick Ngowi, (EA Young Business Leader), na Ofisa Mtendaji wa Techno Brain Ltd, Manoj Shanker, (Entrepreneur of the Year).

WALIOKUFA KWENYE KANISA LA NABII TB JOSHUA WAFIKIA 50!


Idadi ya watu waliokufa kwenye ghorofa la makao makuu ya Kanisa la SCOAN (Synagogue Church of All Nations) la Nabii TB Joshua wamefikia 50.
Jengo hilo la ghorofa tano ambalo ni makao makuu ya kanisa na nyumba ya kulala wageni liliporomoka Jumamosi  wakati ujenzi ukiendelea.Hadi kufikia jana Jumapili jumla ya watu 41 walikuwa wameripotiwa kufa, lakini maiti nyingine tisa zimeongezeka leo hii.Inaelezwa kwamba, mhubiri huyo wa kimataifa alipewa kibali cha kujenga ghorofa mbili, lakini mwenyewe akaamua kujenga ghorofa tano.Uokoaji bado unaendelea na watu wengine 124 walikuwa wameokolewa wakiwa hai hadi kufikia jana Jumapili.
A photo taken and released by Nigeria's National Emergency Management Agency (NEMA) on September 12, 2014 shows emergency workers transporting a man after he was pulled out from the rubble of The Synagogue Church of All Nations
Mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kanisa hilo akiwa hajitambui.
Jengo hilo liko katika eneo la Ikotun magharibi mwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lagos. 
 

LAGOS –

SERIKALI YASEMA BUNGE MAALUM LA KATIBA LINA UHALALI KISHERIA NA KISIASA KUENDELEA


Asha-Rose-300x257Na Magreth Kinabo,Dodoma
Serikali imesema kwamba Bunge Maalum la Katiba linaendelea kwa mujibu wa Sheria, mjadala wa hoja ya kusitishwa kwa Bunge hilo, umefungwa rasmi leo.
Aidha Serikali imewaondoa hofu wananchi kwamba hakuna mgogoro wa kisiasa, hivyo waendelee na shughuli zao za kujipatia kipato(riziki) kama kawaida, pia ipo macho kupitia vyombo vyake vya usalama,itasimamia sheria na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu.
 
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha  Rose  Migiro kwenye kikao cha Arobaini cha Bunge hilo wakati akitoa tamko la Serikali  kwenye mjadala wa mwisho wa kujadili sura zote 15 zilizobakia za Rasimu ya Katiba Mpya.
 
“Bunge hili linaweza kuendelea na shughuli zake. Nawaomba Watanzania wafahamu mjadala wa kusitisha Bunge umehitimishwa hii leo kisheria na Mahakama Kuu ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Dk. Migiro.
 
Dk. Migiro aliongeza kuwa  kwa taarifa walizonazo majadiliano baina na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) pamoja na vyama vyote husika yataendelea Septemba 17 na 18, mwaka huu, kwa sababu mchakato huo si wa chama kimoja, wala viwili au vitatu , bali  mchakato wa Watanzania wote kupitia mfumo ambao umewekwa  wa vyama vyote kisheria.
 
Akizungumzia kuhusu takwimu za wajumbe wa Bunge hilo, Dkt. Migiro alisema  kuwa lina wajumbe 630, kati yao waliotoka nje ya Bunge hilo ni wajumbe 130 ni sawa na asilimia 21 ya wajumbe wote.
 
“Wajumbe waliobakia ndani ya Bunge hili ni 500, sawa na asilimia 79 ya wajumbe wote, tukitazama mambo ya takwimu kwa  kutambua Kundi la 201. Imejitokeza dhana kwamba wajumbe waliobakia humu ndani ni wa aina moja, hiyo si kweli,”alisema.
 
Dk. Migiro alisema  kati ya wajumbe 500, waliobaki katika Bunge hilo, 189, wanatoka katika kundi la 201.
 
Alisema wajumbe  wengine waliobakia, 348 wanatoka upande wa Tanzania Bara, kati ya hao, wajumbe 125 ni wajumbe wanaotoka Kundi la 201.
 
“ Tukiangalia upande wa Zanzibar wajumbe waliobakia ni 152, kati yao wajumbe 64 wanatoka Kundi la 201.Tungependa kusisitiza Kundi la 201 ndio wajumbe ambao kwa wingi wao kitakwimu na kimakundi wanawakilisha Taifa  letu  kwa sura zote.
 
“ Ni dhahiri waliobakia humu ndani ni wengi, hii ina maana kwamba kwa kuzingatia matakwa ya masuala ya kisheria kwa maridhiano, kwa majadialiano na kwa kushawishi hoja.
 
“Wajumbe waliobakia  ni wengi wana uhalali kisheria na kisiasa. Tutaendelea na shughuli zetu kama sheria inavyotutaka, uwakilishi wa Bunge umetimia …  tuna wajibu  wa kisheria wa kufanya  yale tunayoyataka kuyafanya,” alisisitiza  huku akisema waliotoka nje  kwa pande zote mbili hawafikii theluthi moja.
 
Alifafanua kuwa vyama vilivyotoka nje ya Bunge hilo, ni vitatu,vilivyobakia  ndani ya ni 18 ambavyo vimesimamia na vinaendelea kusimamia umoja wa kitaifa  wa nchi yetu.
 
Akichangia mara baada ya tamko hilo, mjumbe wa Bunge hilo, John Shibuda alimpongeza mtoa taarifa hiyo ya Serikali na kuipongeza Serikali kwa kushinda kesi.
Aliwataka Watanzania kuchuja kati ya siasa na maslahi binafsi.