Serikali
imesema kwamba Bunge Maalum la Katiba linaendelea kwa mujibu wa Sheria,
mjadala wa hoja ya kusitishwa kwa Bunge hilo, umefungwa rasmi leo.
Aidha
Serikali imewaondoa hofu wananchi kwamba hakuna mgogoro wa kisiasa,
hivyo waendelee na shughuli zao za kujipatia kipato(riziki) kama
kawaida, pia ipo macho kupitia vyombo vyake vya usalama,itasimamia
sheria na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha taifa linaendelea kuwa na
amani na utulivu.
Kauli
hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria,
Dkt. Asha Rose Migiro kwenye kikao cha Arobaini cha Bunge hilo wakati
akitoa tamko la Serikali kwenye mjadala wa mwisho wa kujadili sura zote
15 zilizobakia za Rasimu ya Katiba Mpya.
“Bunge
hili linaweza kuendelea na shughuli zake. Nawaomba Watanzania wafahamu
mjadala wa kusitisha Bunge umehitimishwa hii leo kisheria na Mahakama
Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Dk. Migiro.
Dk.
Migiro aliongeza kuwa kwa taarifa walizonazo majadiliano baina na
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) pamoja na vyama vyote
husika yataendelea Septemba 17 na 18, mwaka huu, kwa sababu mchakato huo
si wa chama kimoja, wala viwili au vitatu , bali mchakato wa
Watanzania wote kupitia mfumo ambao umewekwa wa vyama vyote kisheria.
Akizungumzia
kuhusu takwimu za wajumbe wa Bunge hilo, Dkt. Migiro alisema kuwa lina
wajumbe 630, kati yao waliotoka nje ya Bunge hilo ni wajumbe 130 ni
sawa na asilimia 21 ya wajumbe wote.
“Wajumbe
waliobakia ndani ya Bunge hili ni 500, sawa na asilimia 79 ya wajumbe
wote, tukitazama mambo ya takwimu kwa kutambua Kundi la 201.
Imejitokeza dhana kwamba wajumbe waliobakia humu ndani ni wa aina moja,
hiyo si kweli,”alisema.
Dk. Migiro alisema kati ya wajumbe 500, waliobaki katika Bunge hilo, 189, wanatoka katika kundi la 201.
Alisema
wajumbe wengine waliobakia, 348 wanatoka upande wa Tanzania Bara, kati
ya hao, wajumbe 125 ni wajumbe wanaotoka Kundi la 201.
“
Tukiangalia upande wa Zanzibar wajumbe waliobakia ni 152, kati yao
wajumbe 64 wanatoka Kundi la 201.Tungependa kusisitiza Kundi la 201 ndio
wajumbe ambao kwa wingi wao kitakwimu na kimakundi wanawakilisha Taifa
letu kwa sura zote.
“
Ni dhahiri waliobakia humu ndani ni wengi, hii ina maana kwamba kwa
kuzingatia matakwa ya masuala ya kisheria kwa maridhiano, kwa
majadialiano na kwa kushawishi hoja.
“Wajumbe
waliobakia ni wengi wana uhalali kisheria na kisiasa. Tutaendelea na
shughuli zetu kama sheria inavyotutaka, uwakilishi wa Bunge umetimia …
tuna wajibu wa kisheria wa kufanya yale tunayoyataka kuyafanya,”
alisisitiza huku akisema waliotoka nje kwa pande zote mbili hawafikii
theluthi moja.
Alifafanua
kuwa vyama vilivyotoka nje ya Bunge hilo, ni vitatu,vilivyobakia ndani
ya ni 18 ambavyo vimesimamia na vinaendelea kusimamia umoja wa kitaifa
wa nchi yetu.
Akichangia
mara baada ya tamko hilo, mjumbe wa Bunge hilo, John Shibuda
alimpongeza mtoa taarifa hiyo ya Serikali na kuipongeza Serikali kwa
kushinda kesi.
Aliwataka Watanzania kuchuja kati ya siasa na maslahi binafsi.
No comments:
Post a Comment