Idadi
ya watu waliokufa kwenye ghorofa la makao makuu ya Kanisa la SCOAN
(Synagogue Church of All Nations) la Nabii TB Joshua wamefikia 50.
Jengo
hilo la ghorofa tano ambalo ni makao makuu ya kanisa na nyumba ya kulala
wageni liliporomoka Jumamosi wakati ujenzi ukiendelea.Hadi kufikia
jana Jumapili jumla ya watu 41 walikuwa wameripotiwa kufa, lakini maiti
nyingine tisa zimeongezeka leo hii.Inaelezwa kwamba, mhubiri huyo wa
kimataifa alipewa kibali cha kujenga ghorofa mbili, lakini mwenyewe
akaamua kujenga ghorofa tano.Uokoaji bado unaendelea na watu wengine 124
walikuwa wameokolewa wakiwa hai hadi kufikia jana Jumapili.
Mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kanisa hilo akiwa hajitambui.
LAGOS –
No comments:
Post a Comment