Sunday, October 12, 2014

JINA LA MJUMBE WA NCCR LAKUTWA KWA WALIOPIGA KURA,MJUMBE AZIMIA MBELE YA WANAHABARI



Na Karoli Vinsent
 Chama Cha NCCR mageuzi kuibuka na kufichua kutokana na kumuorodhesha Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama Cha NCCR-Mageuzi Zanzibar Ndugu Haji Ambar Khamis kuwa Miongozi mwa wajumbe walioshiriki kupitisha katiba hiyo iliyopendekezwa huko yeye akuwepo wala akushiriki vikao hivyo.
           Hayo yameibuliwa Jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo Mbatia alisema chama hicho kilipopata taarifa za kuorodhesha kwa Mjumbe huyo kuhusu kupitisha Rasimu ya Bunge ndipo wakafanya uchunguzi ikiwemo na kumwita Ndugu Haji Ambar Khamisi ili kupata ukweli.
      
        “Tumechunguza na Kubaini kwamba Ndugu   Haji Khamis,ametuthibitishia kwa dhati kwamba hakuwahi kushiriki katika kuandaa wala kupitisha katiba iliyopedekezwa tangu bunge hilo liliporejea kwa mara ya pili tarehe 05 agosta 2014.”

        “ Na kitendao cha kuandika jina la kiongozi wetu wa Taifa katika katiba iliyopendekezwa bila ridhaa yake ni ulaghai uliokithiri kwa watanzania na Dunia kwa ujumla kwani kitendo hicho ni cha udhalilishaji kwa yeye binafisi,Familia yake chama chetu pamoja na viongozi wanachama wote wa Umoja wa kutetea katiba ya wanachi UKAWA na watanzania”Alisema Mbatia.
     
          Mbatia alizidi kusema chama hicho kimeamini kitendo hicho kimefanywa kwa makusidi na Viongozi wakuu wa Bunge Maalum la Katiba ili kukidhi haja zao Binafsi na kulaghai umma wa Watanzania na kusema ni ishara hatarishi kwa usalama wa Taifa letu kwani kitendo hicho kinaweza kusababisha machafuko.
        
       Aliongeza kuwa Uongozi wa NCCR-Mageuzi umepokea katiba iliyopendekezwa kwa Fedheha na Mshtuko mkubwa na kuamini kuwa kuna mkakati mbaya wa kusambaratisha chama hicho kinachokua kwa kasi nchini.
          
        Aidha,Mbatia alisema kwa sasa Chama chake hakitaweza kuvumilia uongo na Uzushi aliufanya mwenyikiti wa Bunge Maalum La katiba katika kupata Thelusi 2 kwa upande wa Zanzibar kwa kufoji wajumbe ambao hawakuwepo kwenye bunge hilo na kusema kwa sasa chama hicho tayari kimewasiliana na wanasheria ili kwenda mahakamaini ili hujuma hiyo igundulike.
        
           Kwa upande wake ndugu Haji Ambar Khamis alisema anashangaa sana kwa kutajwa katika wajumbe walioshiriki kupiga kura kuipitisha rasimu ya bunge na kusema hajawai kuwepo wala kushiriki katika bunge hilo.
      
          “Yaani nashangaa sana maana nimekuwa siishi kwa raha napigiwa simu za vitisho kutoka sehumu mbalimbali na kusema ukweli jamini mimi sijawai kuwepo kwenye Bunge la katiba tangu tulivyosusia vikao hivyo na huu umoja wetu wa UKAWA nashangaa sana leo natajwa mimi kuwepo jamani huu ni uongo mkubwa sana mimi sikuwepo”alisema Khamisi
    
          Katika hali isiyokuwa ya Kawaida Wakati Haji Ambar Khamisi akiwa akijielezea alishindwa kabisa na kuanza kulia na kusema Familia yake ipo katika hali mbaya pamoja na  yeye kutokana na hali ya kisiasa Visiwani Zanzibar kuanza kuchafuka na uwenda familia yake ikauliwa.
       
           Baada ya kusema maneno hali ikazidi kuwa mbaya na akapata mshutuko huku kikao hicho na Waandishi wa Habari kikasimamishwa


na kumkimbiza Haraka Hospitali ya Amana iliyoko Jijini hapa kupata Matibabu.

       
            Baada ya Hali hiyo kutokea ndipo Mwenyekiti wa Chama hicho James Mbatia aliitaka Serikali impe ulinzi Mjumbe huyo huku ikizingatia undani wa suala lenyewe na akakumbushia Mauaji ya Kikatili na yakinyama aliyofanyiwa aliyekuwa mjumbe wa iliyokuwa tume ya marekebisho ya katiba Marehemu Dkt Edmund Mvungi na kusema uwenda unyama huo ukamkuta makumu huyo mwenyekiti. NA ITV

AJALI MBAYA YA BASI LA HAPPY NATION NA GARI NDOGO

 Pichani juu ni baadhi ya Watu wakitazama ajali iliyotokea maeneo ya Hedaru Wilayani Same mkoani Kilimanjaro jioni ya leo,ambapo ajali hiyo ilihusisha gari ndogo yenye namba za usajili T653 BZR kuingia chini ya uvungu wa basi la abairia lijulikanalo kwa jina la Happy Nation,kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa abiria wote waliokuwemo ndani ya gari ndogo (ambao idadi yao haikujulikana) walipoteza maisha papo hapo.Aidha bado haikufahamika mapema chanzo cha ajali hiyo ni nini




MWANAFUNZI CHUO CHA UHASIBU AJICHOMA KISU



Mwanafunzi aliefahamika kwa jina moja la Moza alie mwaka wa kwanza katika chuo cha Uhasibu TIA Mkoani Singida amenusurika kufa baada ya jaribio la kutaka kujiua kwa kujichoma na kisu kushindikana,tukio hilo limetokea jana baada mwanafunzi huyo kumfumania mpenzi wake wa kiume akiwa na mwanamke mwingine.

MABOMU YATIKISA TABATA JIJINI DAR

Askari wa jiji wakiwapakia wafanyabiashara kwenye ‘Karandinga’ ya askari polisi. 
Baada ya kupigwa mabomu ya machozi.
Wananchi wakikimbia.
Mwenye mkoba haya, mwenye mtoto twende…!!
Jamaa akifuta machozi.
Mama mwenye mtoto akinawa maji usoni, pembeni vijana wakinawishana.
Vuta nikuvute ya kutafuta maji ya kunawa.
Gari la polisi likielekea eneo la tukio kuongeza nguvu.ASKARI wa jiji jana walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu wanaofanya biashara kandokando mwa barabara ‘Machinga’ katika maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, aliyezungumza , alifafanua chanzo cha askari kutumia nguvu hiyo, ambapo alisema ni baada ya wananchi kuwapiga mawe wakati wakitekeleza zoezi lao. 
“Majuzi askari wa jiji walikwenda maeneo ya Segerea kwa ajili ya kufanya oparesheni ya kuwaondoa wafanya biashara kandokando mwa barabara, wananchi wakaanza kuwapiga mawe na kufanya zoezi hilo kuwa gumu. Ndiyo maana leo baada ya kuanza kupigwa mawe, nao wakaamua kutumia mabomu ya machozi katika kuwatawanya.’’

Friday, October 10, 2014

AJALI ZA BARABARANI ZAZIDI KUWAMALIZA WATANZANIA








Gari ya Dar Xpress lifanyalo safari zake Kati ya Dar - Rombo likiwa limepata ajali jana jioni eneo la Marangu _Mamba. Watu kadhaa walijeruhiwa
 
 NA HUKO TABORA BASI LA NBS LAPINDUKA BAADA YA KUGONGA PUNDA

 

Habari zilizotufikia  kutoka mkoani Tabora ni kwamba basi la NBS lililokuwa linatoka jijini ,Mwanza kwenda Mpanda,limegonga punda leo asubuhi na kupinduka katika eneo la Nzega Ndogo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia ni kwamba mtu mmoja,ambaye ni kondakta wa basi hilo amefariki dunia na majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega.Inaelezwa kuwa majeruhi 12 wako mahututi

 

TUNDU LISU AKERWA NA UONGOZI WA CHADEMA


Mwenyekiti CHADEMA jimbo la kanda ya kati, Tundu Lissu, akihutubia wana CHADEMA na baadhi ya wakazi wa manispaa ya Singida kwenye viwanja vya Peoples mjini Singida.Tundu pamoja na mambo mengine, amewahimiza wananchi kuikataa rasimu ya katiba mpya kwa madai kwamba imechakachuliwa.
Na Nathaniel Limu, Singida
IDADI  ndogo ya wanachama na wasio wanachama wa CHADEMA waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya mwenyekiti wa jimbo la kanda ya kati, Tundu Lissu, kuzungumza nao, ilimuudhi mgeni huyo rasmi na kutangaza kwamba viongozi wa CHADEMA Manispaa ya Singida, hawana sifa ya uongozi.
Tundu akionyesha kukerwa mno na mahudhurio hayo, alisema wananchi wa mji wa SIngida kwa kipindi cha miaka sita, hawajapata viongozi wanaowastahiki.
“Haya maneno yaliyosemwa na viongozi wa CHADEMA manispaa ya Singida, kwamba wananachi wa mji huu, ni waoga kuhudhuria mikutano ya CHADEMA, ni blaa blaa tupu na hayana ukweli wo wote.
  Ningejua hali ingekuwa hivi, nisingekuja”,alisema kwa masikitiko.
Alisema wananchi wa manispaa ya Singida toka CHADEMA izaliwe, hawajawahi kupata viongozi wenye uwezo bora wa kuongoza, kuhamasisha na kuwaambia ukweli wa mambo yanayoendelea.
DSC00993
Akifafanua zaidi, Tundu alisema wananchi wa manispaa ya Singida, sio waoga kuhudhuria mikutano ya CHADEMA.  Mahudhurio mabovu ya leo, ni matunda ya maandalizi mabovu yaliyofanywa na viongozi wasio na sifa.
Katika hatua nyingine, Tundu ambaye ni mbunge wa jimbo la Singida mashariki, alitumia muda mwingi kumsifia baba wa taifa hayati Julius Nyerere, kwa kudai kwamba alikuwa ni mtu mwenye akili nyingi na alikuwa mwadilifu na hakuwa  mwizi.
“Mwalimu Julius alikuwa na hekima kweli kweli, lakini hata hivyo alikuwa si Mungu, alikuwa binadamu kama mimi na wewe.  Alikuwa kiongozi safi huwezi kumlingansiha na watoto wake hawa (marais waliomfuata)”,alisema.
DSC00992
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Singida,wakimsikiliza mwenyekiti CHADEMA jimbo la kanda ya kati na mbunge wa jimbo la Singida mashariki, Tundu Lissu, wakati akiwahutubia.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Kuhusu rasimu ya katiba mpya, Tundu alisema rasimu hiyo siyo mpya ni ile ile ya mwaka 1962, isipokuwa imejaa mapambo  mapambo, ili kuwaghilibu wanachi.
“Rasimu ya katiba ingesema rais hana haki ya kumnyang’anya mtu ardhi, rais ni binadamu aliyefanya  makosa kama binadamu wengine, akikosa ashitakiwe. Mawaziri wasitokane na wabunge au iondoe nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya. Hiyo ningesema ni rasmu bora kwa usatawi wa watanzania” na kuongeza;
“Katiba mpya itakuwa ya ovyo kuliko hii ya sasa.  Katiba mpya huko mbele itatupelekea tupigane vita na wazanzibar.Nionavyo mimi ni kwamba Wazanzibar hawataipitisha kabisa, nina hofu na huku bara, bara kumejaa ujinga mwingi, kuna uwezekano mkubwa wa kupitishwa  rasimu hii ya katiba mpya”.

TIZAMA SWAGA ZA SENETA WA KENYA MBUNGE KIJANA

UH 2
Mike Sonko ni yule Mwanasiasa mwenye vituko ambae alipata umaarufu sana toka akiwa mbunge kwa kuwa na swagg zake kivyakevyake, alikua mbunge kijana ambae anaingia na hereni bungeni, blingbling kibao kama cheni na pete kama anavyoonekana ametupia kwenye hii picha hapa juu akiwa sasa ni Seneta wa jiji la Nairobi.Sasa juzi kati Rais Uhuru Kenyatta alikwenda The Hague Uholanzi kwenye Mahakama ya ICC kwa hiyo Wakenya wenzake wanaopinga huo uamuzi wa ICC na kuona ni usumbufu wakajilipia nauli zao ili kwenda kumsupport ambapo Seneta huyu ni mmoja wa waliojilipia na kulipia wengine pia.

Pamoja na Sonko kwenda huko akiwa na dukuduku la kukerwa na maamuzi ya Mahakama hiyo akiitaka imuache Rais wao wa Kenya afanye kazi, aliamua kuvaa tshirt yenye maandishi ya Kiswahili ‘ikiwatusi’ Wazungu kama anavyoonekana kwenye hii picha hapa chini.
Kwenye hizi picha hapa chini anaonekana Seneta wa jiji la Nairobi Mike Sonko akiwa amewasili mahakamani ICC na kikosi chake kisha wakafanya maandamano mafupi kabla ya kumpa support Rais Uhuru kwa kuimba wimbo wa taifa na nyimbo za kizalendo wakati kesi ya Uhuru ikiwa inaendelea Mahakani.
Uh 1
Tayari Rais Uhuru Kenyatta amerejea Kenya jana asubuhi na kupokewa na maelfu ya Wakenya ambao hawakupendezwa na kilichofanywa na Mahakama hiyo.

Muda mfupi tu baada ya kuwasili jana Rais Kenyatta alipiga vijembe Mahakama hiyo kwa kusema ‘Walikua wanafikiria kwamba tutakataa kwenda mi nikawaambiwa ile kitu itakataa kuja huko ni Urais wa Wakenya, tumeenda tumekaa huko masaa matatu hatujaambiwa chochote… hatukufungua mdomo sasa hata nashindwa kujua nilikwenda kufanya nini’
‘Ile kitu hawajafahamu kwa vichwa vyao ni kwamba kama nchi ya Kenya tumetoka safari ndefu, na wasifikiri ya kwamba hatujui ni mahali gani tulifanya makosa, sisi tunawaambia hapana….. tuko na suluhu ya shida zetu’
Sonko 2
UH 3
UH 4