Tuesday, August 5, 2014

DAWA YA UKIMWI MBIONI KUPATIKANA


KUMBE inawezekana! Wanasayansi wapatao 30 duniani waliokuna vichwa kutafuta dawa ya kutibu gonjwa hatari la Ukimwi wamesema hatua waliyofikia ni kujipongeza kwa asilimia mia moja.
Wataalam hao walikutana nchini Marekani hivi karibuni na kusema utafiti wao umeweza kutengeneza vidonge vya kudhibiti kasi ya ugonjwa huo kwenye mwili wa mwanadamu.

Wakiwa chini ya Chama cha Kimataifa cha Ukimwi na Jamii (International Aids Society au IAS), wamesema wanaamini miaka kadhaa mbele kutoka 2014 tiba ya uhakika itapatikana.
Mkurugenzi Mtendaji wa IAS, Dk. Bertrand Audoin alisema mafanikio yaliyopatikana kwa sasa ni dawa za kudhibiti virusi vya ugonjwa huo kuushambulia mwili wa binadamu hata kama virusi vitaendelea kuwepo mwilini.

Alisema kwa sasa wanatafiti namna ya kapata dawa itakayoweza kuangamiza kabisa virusi kwenye mwili wa binadamu.Kwa mujibu wa taarifa, dawa zaidi ya nane za chanjo ya ugonjwa huo zipo kwenye majaribio lakini wanasayansi hao hawajasema lini watazianika.

Mojawapo ya dawa iliyopo kwenye majaribio ni ya Niaid ya nchini humo ambayo ilifanikiwa kutambua chembechembe zinazoweza kidhibiti virusi vya ugonjwa huo hatari kwa zaidi ya asilimia 90.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wataalam hao, kukutana kwao kwenye Jiji la Boston, Marekani ilikuwa ni kwa ajili ya kutoa tamko kwa jamii duniani kuhusu mafanikio waliyofikia.

Dk. Audoin amesema mkakati wao wa kwanza ulikuwa kuhakikisha dawa ya Ukimwi inapatikana katika kipindi cha mwaka 2010/2014 ambapo kweli matumaini yapo.Virusi vya Ukimwi viligunduliwa kwa mara ya kwanza kwenye maabara mwaka 1980 na kuua mamilioni ya watu kutokana na kutokuwa na tiba wala chanjo ya uhakika.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi lilipiga hodi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutaka kusikia wanasemaje kuhusu mafanikio ya chanjo na tiba ya Ukimwi yaliyoanza kupatikana lakini hakupatikana msemaji.

No comments:

Post a Comment