Tuesday, August 5, 2014

TAHA YATOA ELIMU KWA WAKULIMA WA MBOGAMBOGA KWENYE MAONYESHO YA NANENANE MKOANI MBEYA

Wananchi waa jijini Mbeya na mikoa ya jirani wamepata bahati ya kupata elimu ya bure ya kilimo cha mbogamboga, matunda na viungo kutoka kwa asasi isiyo ya kiserikali ya wakulima,wafanyabiashara na watoa huduma ya mazao ya horticulture tanzania (TAHA)
Elimu hiyo inayotolewa katika banda na vitalu vya maonyesho vilivyopo katika uwanja wa maonyesho wa nanenane wa John Mwakangale jijini Mbeya. Elimu iliyoambatana na  elimu lishe nia ikiwa kuwaelimisha wananchi umuhimu wa mbogamboga na matunda katika lishe na kujipatia kipato kwa kulima mbogamboga na matunda

Wakulima waliotembelea banda hilo wamenufaika na elimu hiyo inayotolewa na maafisa wa ufundi wa kilimo kutoka TAHA kwa ushirikiano na wale wa Barton Tanzania ambao kwa pamoja wapo katika viwanja hivyo ili kuhakikisha jamii ya wakulima wa mboga kutoka ukanda wa Nyanda za Juu Kusini wanapata elimu ya msingi bora ya uzalishaji wa mboga wenye tija. 


"Tumetembelewa na wakulima wasiopungua 500 na bado tunauhakika kuwa watakuja wengi kadiri siku zinavyokwenda kwani hawa waliotutembelea wamefurahia sama mafunzo haya hivyo natumaini watakwenda kupashana habari huko waendako kwani wote waliofika hapa wamefurahia elimu hii" alisema Afisa mawasiliano wa TAHA Likiti Thomas
Aliongeza kuwa wakulima wengi waliotembelea banda hilo wametaka sana  kujifunza mbinu na misingi ya awali ya uzalishaji wa mazao ya horticulture, hiyo ni ishara njema kwani inaonesha ni kiasi gani wananchi  wanatafuta mbinu fasaha inayoweza kuwakwamua kutoka katika uzalishaji wa mboga wa kawaida mpaka uzalishaji wa tija unaozingatia viwango vya kitaifa na kimataifa ili kujipatia manufaa zaidi ya hayo wayapatayo sasa kwani wengi wamegundua kuwa ipo fursa ya kujikwamua kimaishakwa kutumia kilimo
Mkuu wa mkoa wa Iringa  Mh. Dr. Christine Ishengoma akionyeshwa zao la nyanya katika moja ya vitalu vya TAHA


Nae mtaalamu wa kilimo Bwana Ringo amesema elimu itolewayo ni pamoja na matumizi ya mbegu bora (hybrid) pamoja na teknolojia za kisasa kwa ajili ya uzalishaji bora wa mazao. "katika maonyesho ya mwaka huu tupo kivitendo zaidi kwani mkulima anapata mafunzo kwa kusikiliza na kuona pia kwa kujenga imazi zaidi na kumpa mkulima hamasa ya kwenda kuyafanyia kazi mafunzo yetu"
 Vitalu vilivyotumiwa kwa ajili ya mafunzo kwa wakulima wa mbogamboga jijini Mbeya

 Mwananchi akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa TAHA
 Teknolojia ya umwagiliaji kwa mfumo wa kilimo cha matone (drip irrigation)ambao pia unaonesha utengenezaji bora wa matuta, nafasi na usafi ambayo huendana na mfumo wa kisayansi na teknolojia



kama ilivyo kauli mbiu ya TAHA ambayo ni "maono ya baadae ndiyo msingi na rasilimali zetu kuhakikisha ufanisi na mafanikio" ambapo nia ni kutaka mkulima kutumia rasilimali alizo nazo kujipatia kipato ikiwa ni pamoja na ardhi kwa ajili ya kilimo kwa kulima mazao tofauti tofauti kwa kutumia shamba moja

No comments:

Post a Comment