Tuesday, August 5, 2014

WATU HAWA SARE WANAZITOA WAPI?



 Askari feki wa Usalama Barabarani ambae Jina lake halikufahamika haraka akiwa chini ya Ulinzi mkali wa Askari Polisi (hayupo pichani) mara baada ya kukamatwa kwa kujifanya ni askari wa usalama barabarani huku akifahamu kuwa ni kosa kisheria. Inasemekana Mtuhumiwa aliwahi kuwa askari wa Usalama barabarani ambapo kituo chake cha Kazi kilikuwa Mkoa wa Pwani na ni mmoja kati ya askari waliofukuzwa kazi kwa kuenda kinyume na taratibu na sheria za Jeshi la Polisi Tanzania
 Askari Polisi ambae jina lake halikufahamika mara moja (Mwenye sweta) akimkamata kwa makini mtuhumiwa aliyejifanya askari wa usalama barabarani leo katika eneo la Chamazi Jijini Dar Es Salaam
Askari feki akishangaa na kuduwaa mara baada ya jeshi la Polisi Kumtia nguvuni leo Katika Eneo la Chamazi Jijini Dar Es Salaam Mapema leo.Picha Kwa Hisani ya Mdau.

No comments:

Post a Comment