Monday, September 29, 2014

KIJANA ACHOMWA MOTO HADI KUFA KWA WIZI


MTU mmoja mwenye umri kati ya miaka 25 na 30 ambaye jina lake halifahamiki, ameuawa baada ya kushindwa kujieleza juu ya pikipiki ambayo yeye na mwenzake walikuwa wanajaribu kuiuza Chalinze.
Watu hao walifika Chalinze wakidai kutokea Gairo wakitaka kuuza pikipiki aina ya Toyo yenye namba za usajili T 336 BZC. 
Lakini walipobanwa kuhusu kadi ya pikipiki walibabaika na hivyo kuanza kupigwa ambapo mmoja alitoroka na huyo mwingine kuuawa kwa kuchomwa moto baada ya kipigo. 
Tukio hilo limethibitishwa na kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Athuman Mwambalaswa.
Kamanda huyo alisema kwamba tukio hilo lilitokea Septemba 25 mwaka huu, majira ya saa 1 asubuhi eneo la Pera Chalinze wilaya ya Bagamoyo.
 
Kamanda huyo aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kuwataka kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria, ikiwa ni pamoja na polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

No comments:

Post a Comment