Monday, September 29, 2014

UVCCM WAMVAA JAJI WARIOBA

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umemtaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba, aingie mtaani kupambana akiwa na chama cha siasa badala ya kuendelea kutumia mwamvuli wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Tamko hilo lilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka  alipozungumza na mjini Dodoma nje ya viwanja vya Bunge mjini hapa .

Shaka alisema anachokifanya sasa Jaji Warioba ni kinyume cha taratibu ziliozompa dhamana awe Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambapo sasa ni dhahiri matamshi yake yanatoa tafsiri ya kutaka ushindani na vyombo vya dola.

“Nampa ushauri wa bure usio na gharama mzee Warioba, akubali kuanzisha chama cha siasa ifahamike ana mchuano na Dola ilio chini ya Rais Kikwete, asitangaze kuingia mitaani kwa kukitumia kivuli cha Tume ya Rais iliofika ukomo wake kisheria”alisema Shaka.

Shaka alisema kimsingi ifahamike kwamba Jaji Warioba mwaka 2005 alijibanza chini ya  kivuli cha Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kutoa kauli hasi dhidi ya viongozi wa serikali.

Shaka alisema si lazima kwa Jaji Warioba kuendelea kubaki kuwa CCM na kwamba ana haki ya kikatiba na kidemokrasia kutoka ili akipinge vizuri chama hicho

No comments:

Post a Comment