Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akimkaribisha wilayani Monduli Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh.
Masaki Okada wakati alipowasili wilayani humo jana Jumapili Septemba
28,2014 kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo
inayofadhiliwa na nchi hiyo.Balozi huyo aliahidi kusaidia vifaa vya
kisasa katika hospitali mpya ya kisasa inayojengwa wilayani humo.
Meneja wa
Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema (kushoto) akimkaribisha
Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada hotelini hapo.Pembeni
kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli,Bw. Twalib
Mbasha.
Balozi wa
Japan nchini,Mh. Masaki Okada (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa
Halmashauri
ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha (kulia) na Meneja wa
Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema alikofikia balozi huyo na
ujumbe wake katika ziara yake ya siku mbili wilayani humo.
No comments:
Post a Comment