Tuesday, September 23, 2014

KIJANA AFUMANIWA NA MWANAFUNZI WA KIUME GESTI

Njemba aliyekutwa na denti akipanda kwenye difenda.
“Mwanzo tulifikiri anakuja na vijana hao kama marafiki zake wa kawaida lakini tukaingiwa na wasiwasi baada ya kugundua kuwa alikuwa akilala nao kwa kuwabadilisha,” alisema meneja huyo.
Alidai kwamba Jumapili iliyopita, majira ya saa 3:00 usiku, kijana huyo alitinga tena kwenye gesti hiyo lakini alikuwa peke yake na kupewa chumba kama kawaida.
“Wahudumu waliniambia kuwa jamaa amefika tena na amechukua chumba cha juu lakini safari hii alifika peke yake, ilinishangaza sana kusikia kaja peke yake kwani siyo kawaida yake so sikuamini,” alieleza meneja huyo.
Alidai kwamba asubuhi ya Jumatatu, mishale ya saa 4:00, wahudumu walisikia miguno ndani ya chumba alicholala njemba huyo ndipo wakakifunga kwa nje kisha kuita polisi na vijana wa OFM ambao walifika eneo la tukio ndani ya ‘dakika sifuri’.
Meneja huyo alisema kuwa hafahamu njemba huyo alimuingiza kijana huyo muda gani kwani walimuwekea mtego siku nyingi akawa anachezwa na machale.
Hata hivyo, Jiji la Dar huwa halina dogo kwani wakazi wa eneo hilo walijazana kwenye gesti hiyo kutaka kumpiga jamaa huyo lakini polisi walifanikiwa kuwatorosha eneo hilo na kuwampeleka Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar.
Hadi OFM inang’oa nanga kituoni hapo, njemba huyo na kijana aliyekutwa naye walikuwa wakiendelea kuhojiwa. Kujua kilichojiri usikose kufuatilia magazeti ya Global.

No comments:

Post a Comment