WANANCHI wa Kata ya Kawetele Tarafa ya Tukuyu mjini wilayani
Rungwe Mkoani Mbeya wanatarajia kufanya
maandamano ya amani hadi kwenye ofisi ya
mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kupinga hatua ya ofisi yao kuwekwa kwenye kirabu
cha pombe.
Wakizungumza jana na
Yetu rungwe blog kwa nyakati
tofauti wamedai kitendo cha ofisi ya serikali kuwa katikati ya kirabu cha pombe
na kumbi za starehe kimeshusha hadhi ya mji wa Tukuyu ambao ndiyo makao makuu
ya wilaya hiyo.
Walida kuwa asilimia ishirini ya wananchi wa kata hiyo ni
walokole hivyo wanakosa kupata huduma za kiofisi kutokana na mazingira mabaya
ya kiofisi yalivyo hivyo hulazimika kupata huduma za kiofisi kwenye kata za
mbali kinyume na taratibu.
Wananchi hao ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini
walisema madai yao yakuomba ofisi kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo
Veronika Kessy yamegonga mwamba na kudai kuwa wamepanga kufanya maandamano ya
amani wakitaka kupatiwa ofisi.
Afisa mtendaji wa Kata hiyo Niklaus Kosama alikiri kuwepo na
hali hiyo na kudai kuwa yeye ameletwa kufanya kazi katika kata hiyo na hana mamlaka ya kupinga ofisi kuwepo
mahali hapo.
Anyimike Mwasakilali diwani wa Kata hiyo mbali na kukiri
kuwepo kwa hali hiyo pia alidai kuwa alipeleka maombi ya kupatiwa ofisi kwa
mwenyekiti wa Halmashauri na mkurugenzi wa halmashauri hiyo lakini alikuwa akipigwa dana dana
Alisema afisa utumishi wilayani humo alimueleza kuwa amempa
barua ya kuhama mtumishi anayeishi nyumba no,RDC/RHB/BLD/08 kuwa mwezi wa 11
mwaka huu mtumishi huyo atahama na nyumba hiyo itafanyika kuwa ofisi ya kata.
Yetu rungwe ilimulika
hadi kwenye nyumba hiyo
kujiridhisha kana kwamba ni kweli mtumishi huyo wa Idara ya maji kama kapewa
barua ya kuhama,ambapo alikanusha kuwa hajawahi kupewa barua ya kuhama na wala
hata kwa mdomo.
Alfredy Mwakipiki mwenyekiti wa Halmasahuri hiyo kwa upande
wake alisema anachokijua ni kuwa wananchi wa kata hiyo walifanya harambee ya
kutaka fedha kwa ajili ya ununuzi wa uwanja na wao watawasapoti pindi watakapo
jenga hadi mtambaa wa panya.
Alisema Halmashauri ya Rungwe magharibi inakata 20 na
imekuwa ikishindwa kujenga kwa wakati ofisi za kata kutokana na bajeti ndogo,hivyo
suala la ofisi katika kata hiyo litapewa kipawa mbele pindi wapatapo bajeti. | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
No comments:
Post a Comment