Tuesday, September 23, 2014

RAPPER WITNESS APOTEZA MAPACHA KWA UJAUZITO WAKE KUHARIBIKA


Rapper wa kike Witness amepata bahati mbaya baada ya ujauzito wake wa miezi nane na nusu kuharibika.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Witness ameeleza kuwa alikuwa anatarajia mapacha na alikuwa katika hatua za mwisho lakini ghafla ikatokea hali hiyo ambayo hadi sasa inafanyiwa uchunguzi na madaktari kubaini chanzo.


“Kuna mambo ambayo niliambiwa kwamba endapo ningekuwa sina mazoezi au ningekuwa siko strong ina maanisha kwamba na mimi mwenyewe ningekuwa hatarini.” Amesema Witness.

Ameeleza kuwa hali hiyo ilitokea Ijumaa iliyopita lakini yeye na mchumba wake Ochu waliamua kukaa kimya kwa muda hadi leo walipoamua kuiweka wazi.

Akiongelea afya yake, member huyo wa zamani wa WAKILISHA ameeleza kuwa hivi sasa anaendelea vizuri.

Tunampa pole kwa tatizo hilo lililomkuta na tunamuombea awe na afya njema kama zamani.

No comments:

Post a Comment