Tukio hili limetokea
eneo la Bonanza kata ya Chamwino, Dodoma mjini. Kwa shuhuda wetu
aliyekuwa eneo la tukio amesema kuwa dereva wa bodaboda amekutwa
amefariki baada ya kuuliwa na watu wasiojulikana na kisha watu hao
kutoweka bodaboda aliyokuwa akiendesha marehemu huyo. Dereva huyo wa
bodaboda amechomwa kisu maeneo ya tumboni na shingoni katika mwili wake
na katika eneo la tukio kumekutwa visu viwili amavyo vinasadikika
kutumiwa katika uharifu huo kando kidogo ya barabara na sehemu ulipokuwa
mwili wa marehemu.(Picha na Alex wa Pamoja Blog)
Hiki
ni mojawapo ya kisu kinachosadikiwaa kutumika katika kufanya mauaji
hayo ya dereva wa Bodaboda na kisha watu hao kutoweka na pikipiki.
No comments:
Post a Comment