Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, ameibuka mshindi wa tuzo
mbili kwenye fainali ya shindano la kuwania Tuzo ya Mwaka ya
Mfanyabiashara Bora Afrika (AABLA) kundi la Afrika Mashariki.
Sherehe za kutoa tuzo hizo zilifanyika jijini Nairobi, Kenya Jumamosi iliyopita.
Dk. Mengi alitunukiwa Tuzo ya Mfanyabiashara Bora Afrika kwa mwaka 2014,
kutoka kundi la Afrika Mashariki. Majaji wa shindano hilo pia waliamua
kumtunuku Tuzo ya Maisha ya Mafanikio kwa kuongoza katika suala la
uwajibikaji kwa jamii.
Dk. Mengi ambaye pia liingia kwenye kurasa za gazeti maarufu la Forbes
Africa la Julai mwaka huu wa 2014, amekuwa akichangia sehemu kubwa ya
muda na rasilimali zake kwa ajili ya kufadhili kazi zinazogusa maisha ya
jamii.
Kwa upande wa Tuzo ya Kijana Mfanyabiashara Kiongozi wa Mwaka, tuzo hiyo
ilienda kwa Patrick Ngowi, CEO wa Helvetic Solar anayeongoza kampuni
inayokua kwa kasi kwenye mtandao wa nishati mbadala katika ukanda wa
Afrika Mashariki.
Anaongoza wafanyakazi zaidi ya 300, akichangia kwenye ukuaji na
maendeleo yanayolenga mipango ya kibiashara katika taifa la Tanzania na
ukanda mzima wa eneo hili.
No comments:
Post a Comment