My
God! Mama aliyetambulika kwa jina la Swaumu Sadick (25), mkazi wa
Manzese jijini Dar, amejikuta yeye na manesi wakitimua mbio kwa woga
baada ya kujifungua kiumbe wa ajabu.
Swaumu
Sadick akiwa hospitali baada ya kujifungua mtoto huyo. Kwa mujibu wa
shuhuda wetu, tukio hilo ambalo kwa sasa ni gumzo, lilijiri hivi
karibuni mishale ya saa 8:00 usiku kwenye Kituo cha Afya Cha Kijiji cha
Mlali kilichopo wilayani Mvomero mkoani hapa.
Katika tukio hilo, ilielezwa kwamba Swaumu alijifungua kiumbe huyo wa
ajabu anayedaiwa kuwa na mkia mrefu huku akiwa hana miguu.
Ilidaiwa kwamba baada ya kutokea kwa tukio hilo, baadhi ya ndugu
walishikwa na taharuki kubwa huku wengine wakitoa taarifa kwa
mwanahabari wetu ambaye alifunga safari kutoka mjini Morogoro na
kuwasili kwenye kituo hicho cha afya majira ya saa 12:00 asubuhi.
Katika mahojiano maalum na gazeti hili juu ya tukio hilo, nesi wa
zamu aliyekutwa kituoni hapo aliyejitambulisha kwa jina moja la
Consolatha alikuwa na haya ya kusema: “Nilimpokea Swaumu majira ya saa
1:00 usiku akilalamika kuwa na uchungu wa kujifungua.
Swaumu
Sadick akiuguzwa hospitali. “Nilimpa kitanda. Saa 8:00 usiku, uchungu
ulizidi nikampeleka leba ambako alijifungua kiumbe huyo mwenye jinsi ya
kiume. “Baada ya kujifungua na kumuona kiumbe huyu wa ajabu, nilitimua
mbio usiku huo kwa woga na kwenda kuamsha manesi wenzangu wanoishi kota
za kituo hiki cha afya.
“Nimefanya kazi hii ya ukunga na kuzalisha wazazi zaidi ya 50 lakini sijawahi kukutana na tukio kama hili.”
Kwa upande wake mganga mkuu wa kituo hicho aliyejitambulisha kwa jina
moja la Dk. Beatrice alikuwa na haya ya kusema juu ya tukio hilo la
kusikitisha:
“Kimsingi si kiumbe ila ni mtoto ambaye awali tulipomcheki mzazi
tulibaini ana kichwa kikubwa na alishafia tumboni zaidi ya siku
tatu.“Amezaliwa akiwa na miezi nane tumboni. Tulichokifanya ni kuokoa
maisha ya mama jambo ambalo tumefanikiwa.”
Mtoto wa ajabu aliyezaliwa na Swaumu. Akizungumza kwa tabu na
mwanahabari wetu, Swaumu alisema: “Hii ni mimba yangu ya tatu, ya kwanza
iliharibika tumboni, ya pili nilifanikiwa kuzaa salama mwanangu
Maimuna.
“Hii ya tatu ndiyo nimejifungua kitu hiki cha ajabu.”
Alipoulizwa kwa nini aliondoka Dar ambako ndiko kwenye hospitali
kubwa na kwenda kujifungulia kijiji akijua ana matatizo ya uzazi, mama
huyo alisema:
“Siku za kujifungua zilipokaribia mume wangu Abdallah aliniambia nije
kujifungulia kwa bibi yangu Halima, kwa bahati mbaya ndiyo yametokea
haya.”
Kwa upande wake shangazi wa Swaumu aliyekutwa akimhudumia alisema:
“Yameshatokea ya kutokea, tunamshukuru Mungu na tunajiandaa kumchukua
mjukuu wetu tukamzike.”
No comments:
Post a Comment