Jenerali James Kok ambaye ni Mjumbe wa
kamati kuu, SPLM, Mbunge , amewahi kuwa Waziri wa masuala ya kijamiii na
bisahara katika serikali ya umoja wa kitaifa Sudan,SPLM - IG
akiwasalimu wananchi wa Masasi. Msafara wa viongozi hao kutoka Sudani
kusini ulifika wilayani Masasi kwa lengo la kufanya mazungumzo na Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana (mwenye shati la kijani) pamoja na viongozi wa chama cha SPLM
kutoka Sudani Kusini wakiwa wameinua mikono juu kama ishara ya umoja na
mshikamano,Masasi mkoani Mtwara.
Kutoka Kushoto ni Dkt. Cirino Hiteng,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Bw.Goy Jooyul na Jenerali James Kok.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa chama cha SPLM kutoka
Sudani ya kusini waliomfuata Masasi mkoani Mtwara ambapo Katibu Mkuu wa
CCM yupo kwenye ziara ya kukijenga na kukiimarisha chama mkoani Mtwara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akimsikiliza Jenerali James Kok kutoka chama cha SPLM Sudani ya Kusini
ambaye yeye pamoja na viongozi wenzake wamefika mpaka Masasi kufanya
mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM
No comments:
Post a Comment