Matukio ya
mimba za utotoni yamekuwa yakijitokeza kila kukicha yakiwa na sura
tofauti, mengi yametajwa kuharibu maisha na kupoteza ndoto za wasichana
wengi.
Kutoka
Nigeria Mzee mwenye umri wa miaka 75 anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa
kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13.Mzee huyo Pa
Alabi ambaye ni fundi seremala aliombwa na binti huyo kumtengenezea
kiboksi cha kuhifadhia pesa zake, baada ya kumpa kiboksi hicho akaanza
kumtongoza na kujenga ukaribu nae hadi binti akakubali.
“..Siku yenyewe nilimwelezea hisia zangu na akaahidi kulifikiria
suala hilo na baadae akakubali, tulikutana kimwili pale nilipomuomba na
tulikuwa tukiheshimiana, ghafla akaacha kuja kwangu baada ya siku tano
baada ya ile siku ya kwanza tulipokutana kimwili. Siku moja akaja na
kuniambia Bibi yake alimwambia ni mjamzito ndipo alipoacha kuja kwangu
na sikumuona tena hadi Polisi walipokuja kunikamata..– Pa Alabi.
Siku ya kwanza msichana huyo kukutana na Alabi alimpatia hela Naira
200 na kumnunulia simu ya mkononi yenye thamani ya Naira 150 pesa za
Nigeria na baada ya kukamatwa na kuhojiwa alijitetea kuwa hakujua kama
ni kosa kukutana kimwili na binti huyo mdogo na kueleza kuwa lengo lake
ilikuwa ni kumuoa na kumtunza yeye na mtoto wake.
No comments:
Post a Comment