Wanaume
nchini Kenya wameelezea hisia mseto kuhusu wito wa kiongozi wa Shirika
la Maendeleo la Wanaume nchini humo kwamba hapo kesho tarehe 11 wasusie
tendo la ndoa na kuonyesha hisia za mapenzi kwa wanawake.
Wiki jana
kiongozi huyo Nderitu Njoka amewataka wanaume nchini Kenya kufanya hivyo
kuadhimisha siku ya kimataifa ya uhuru kwa wanaume inayoadhimishwa kila
mwaka tarehe 11 mwezi Novemba.
Bwana
Nderitu amewataka wanaume wote kutojihusisha na wanawake kimwili , wawe
wameoa au la kama ishara ya kuonyesha ghadhabu yao kwa ongezeko la
dhuluma wanazotendewa wanaume pamoja na ongezeko la utumiaji wa dawa za
kulevya na pombe miongoni mwa wanawake.
Wito huo
hata hivyo umepuuzwa na baadhi ya wanaume ukitajwa kuwa njama ya bwana
Nderitu kujipa umaarufu katika vyombo vya habari.
Hatua hiyo
pia inatumiwa kjuonyesha kero la wanaume kutokana na hatua ya serikali
kutenga shilingi bilioni mbili kwa mahitaji ya wasichana wakati ikikosa
kutoa mchango kama huo katika kusadia wanaume wengi kufanyiwa tohara.
Njoka
alinukuliwa akisema kuwa kidini wanaume ndio vipngozi wa familia lakini
leo wamedhalilishwa huku wanawake wakitawala dunia.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment