Monday, November 10, 2014

AJALI YA NDEGE YACHUKUA UHAI WA DK MUNROE


Dk. Myles Munroea akiwa na mkewe Ruth enzi za uhai wao.
KIONGOZI wa Bahamas Faith Ministries, Dk. Myles Munroe, mkewe Ruth na watu wengine saba wamefariki dunia katika ajali ya ndege jana huko Bahamas.

Dk. Myles Munroe (kulia) wakati akiwa jijini Dar Oktaba mwaka huu akitazama vitabu vya mtunzi na mwalimu wa ujasiriamali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo…

Dk. Myles Munroea akiwa na mkewe Ruth enzi za uhai wao.
KIONGOZI wa Bahamas Faith Ministries, Dk. Myles Munroe, mkewe Ruth na watu wengine saba wamefariki dunia katika ajali ya ndege jana huko Bahamas.

Dk. Myles Munroe (kulia) wakati akiwa jijini Dar Oktaba mwaka huu akitazama vitabu vya mtunzi na mwalimu wa ujasiriamali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo (katikati). 
Katika ajali hiyo, ndege ndogo waliyokuwa wakisafiria iligonga winchi na kulipuka wakati ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Grand Bahama.
Dk. Myles Munroe wakati akiendesha mkutano wa viongozi wa serikali, wafanyabiashara na viongozi wa makanisa Oktoba mwaka huu jijini Dar.
Dk. Munroe ambaye pia alikuwa mzungumzaji maarufu wa mambo ya uongozi na biashara duniani, Oktoba 21, mwaka huu alitoa somo kwa viongozi mbalimbali nchini katika mkutano wake mkubwa uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar.

Dk. Munroe akiwa nchini Tanzania mwezi Oktoba mwaka huu.
Katika mkutano huo, Dk. Munroe kutoka Nassau, Bahamas, alifundisha mbinu za kuwafanya viongozi waweze kuchanganua mambo, kutimiza majukumu yao na hatimaye kufikia malengo makubwa ya kimafanikio ambayo yanaweza kuifanya nchi ipige hatua.
Dk. Myles Munroe akisalimiana na Eric Shigongo walipokutana katika Hoteli ya Serena jijini Dar, Oktoba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment