Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando wakati akifanya yake.
Mapema wiki hii, chanzo kimoja kilipiga simu katika chumba chetu cha habari na kusimulia kuhusu habari hiyo, kwamba, Rose ambaye hana mume, amenasa na muda wowote kuanzia sasa anaweza kuitwa mama.
Madai ya chanzo hicho yalieleza kwamba, staa huyo amekuwa akijichimbia nyumbani kwake mkoani Dodoma tofauti na siku za nyuma ambapo alikuwa hakauki jijini Dar.
“Kama hamsadiki ninayowaambia, najua ninyi mmebobea kwenye habari za uchunguzi ‘so’ fanyeni yenu mtaniambia,” kilidai chanzo hicho kikiomba chondechonde kisichorwe jina gazetini.
Ili kujiridhisha na habari hiyo, pasipo kwanza kuwasiliana na Rose, moja kwa moja, gazeti hili lilimpigia simu mmoja wa watu wa karibu wa nyota huyo (jina linahifadhiwa), alipopatikana, aliulizwa kuhusu ishu hiyo na haya ndiyo aliyoyaeleza:
Rose Muhando akipafomu na madansa wake.
“Yaani hadi leo mlikuwa hamjapata hii habari? Mimi siku zote nilikuwa najua labda kwenu siyo habari kwa sababu ujauzito huu ni wa siku nyingi. “Hata sasa hivi ukimuona alivyo unajua wazi kuwa kuna kichanga tumboni kwani tumbo limechomoza hatari.”
Mtu huyo wa karibu alisema anapokuwa nyumbani Dodoma mara nyingi amekuwa mtu wa kukaa ndani tu kutokana na watu kumshangaa.Alisema Rose amekuwa akijificha kwa sababu ya kuogopa macho ya watu na uchovu unaotokana na hali aliyonayo ‘kuchoka’.
NANI MHUSIKA?
Juu ya nani mhusika wa mimba hiyo, mtu huyo wa karibu, ambaye anafahamu kila kinachofanywa na nyota huyo wa Wimbo wa Facebook alisema kuwa, inadhaniwa kuwa ni ya mcheza shoo wake (jina kapuni).
Inadaiwa kwamba, Rose, mara kadhaa amekuwa akisisitiza kuwa ni lazima amzalie mtoto jamaa huyo kwa jinsi anavyompenda.“Huyo mcheza shoo ana uhusiano naye kwa muda mrefu kidogo na ameshasema kwa watu wengi tu kwamba endapo Mungu atapenda basi atafurahi kama atamzalia mtoto.
“Mimi hajaniambia mimba hasa ni ya nani, lakini naziona dalili zote kuwa ni ya huyo kijana,” alisema mtu huyo.Rose Muhando na madansa wake wakitoa burudani.
Baada ya kujiridhisha na maelezo ya mtu wake wa karibu, gazeti hili lilianza kumtafuta Rose, mama wa watoto watatu ambao wote amezaa na wanaume tofauti, lakini katika hali ya kushangaza, simu yake iliita hadi kukatika bila kupokelewa, hata baada ya kupigwa mara kadhaa.
Likiamini huenda alikuwa katika shughuli au mahali panapombana kuzungumza, gazeti hili lilimtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na kumsomea mashitaka hayo ili atoe ufafanuzi, lakini pia hakuweza kujibu.
Likiamini huenda simu yake haisomeki kwa mtumishi huyo wa Mungu, gazeti hili lilitumia simu nyingine ambayo nayo iliita kwa muda mrefu hadi kukatika pasipo kupokelewa na hata pia alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu wenye maelezo kuhusu hali yake ya sasa, pia haukujibiwa hivyo jitihada zinaendelea.
Endapo itathibitika, ujauzito wa Rose utakuwa ni wa mtoto wa nne ambapo mara kadhaa staa huyo amekuwa akisema hayupo tayari kuolewa hivyo kuwaacha baadhi ya watumishi midomo wazi wakiamini mtu wa sampuli yake haifai kuzaa nje ya ndoa.