Monday, December 1, 2014

MWANAJESHI ALEWA CHAKARI MPAKA KUZIMA


 Wananchi Iringa wakimtazama askari wa jeshi ambae jina halikuweza kufahamika aliyekuwa amezima kwa ulevi uliopinduki
 mjeshi huyo akiwa akiwa amezima
 Mjeshi huyo akiwa amepata fahamu baada ya kumwagiwa maji
Mjeshi akiwa amezima kwa kunywa pombe kupita kiasi
KATIKA hali isiyotegemewa askari mmoja wa jeshi la kujenga Taifa (JKT) anayesadikika kuwa na wa kambi ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa usiku wa juzi amenusurika kuvuliwa nguo za jeshi hadharani baada ya kukutwa amelewa chakali na kulala katika mfereji wa maji machafu eneo la nje ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa


Tukio hilo lilitokea muda wa saa 2 usiku baada ya wasamaria wema kumshusha askari huyo kutoka katika basi la Mgumba ambalo alikuwa amepanda kutoka Mafinga kuja mjini Iringa.

Akisimulia kisa na mkasa wa askari huyo kulewa chakali kiasi cha kushindwa kujitambua mmoja kati ya wasamaria wema aliyejitolea kumshusha katika basi hilo alisema kuwa askari huyo alipanda basi hilo Mafinga huku akiwa amelewa na wakati wote wa safari alionekana akinywa pombe kali kiasi cha kushindwa kujimudu na kuanza kutapika na kujisaidia haja ndogondani ya basi hilo.

Hata hivyo alisema baada ya kufika stendi ilikuwa ni vigumu kujitambua hivyo kupoteza fahamu na kulazimika kumpa msaada na kumzimua kwa maji kabla ya kupata fahamu kiasi na kujificha chini ya mfereji wa maji machafu .

Alisema kuwa mara baada ya kujitambua kiasi aliweza kutoa namba ya ndugu yake ambae ni askari wa FFU mjini Iringa aliyefika kumnusuru kuvuliwa nguo na kiongozi wake aliyefika eneo hilo na kumkutana akilishushia heshima jeshi kwa ulevi uliopitiliza

" Umelidhalilisha sana jeshi kwa askari kulewa hivi ukiwa katika sare .....sasa nataka kukuvua sare kisha nakupeleka kulala polisi kabla ya kesho kukuchukulia hatua zaidi " alisikika akisema kiongozi huyo ambae jina wala cheo chake hakukitaja
Maamuzi hayo ya kiongozi wake yaliwafanya mashuhuda kumuangukia na kumwomba amsamehe kwani bado ni kijana mdogo sana mambi ambayo aliyakubali na ndugu zake kumpakiza katika Taxi na kumpeleka eneo la Kihesa 
Ushauri wetu kwa askari wetu kujaribu kuheshimu nafasi hizo japo hakuna anayewakataza kunywa pombe ila watambue kuwa unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako ama chonde chonde ulevi noma.

1 comment:

  1. titanium dab nail - 3/8 - The best and most accurate nail
    Titanium Abits. This one titanium engagement rings is made from the finest aluminium trekz titanium headphones surfaces. This is a perfect titanium paint color razor for a titanium scrap price serious person, 2020 escape titanium especially a beginner and beginner.

    ReplyDelete