Bi Mwadawa ambaye ni mratibu wa makazi katika VICOBA nchini amejitoa muhanga kuwa mwalimu wa wanawake na wanaume ambao wapo tayari kuondokana na umaskini kwa kuwakusanya pamoja na kuwafundisha jinsi ya kuondokana katika hali ya kuwa tegemezi na kuwa wajasiliamali.
Mwanamke huyo ambaye amesema haikuwa kazi rahisi kwake kuwakusanya watu wa fikra tofauti na kuwafundisha kuhusu VICOBA endelevu kitu kilichopelekea yeye kuitwa tapeli na baadhi ya watu. Hata hivyo alisema kuwa hakukatishwa tamaa na watu hao badala yake alifanya juhudi kutoa elimu hiyo kwani alijua kitu anachokifanya.
Bi Mwadawa ambaye sasa anavikundi 33 vya VICOBA na zaidi ya nusu ya vikundi hivyo vimeshajiunga kwenye mpango wa APPEX ambapo vikundi vyote vinauwezo wa kukopesheka kibenki na kujiendeleza.
Bi huyo na kikundi chake cha agape jana walizindua ofisi yao ya VICOBA cha MAKAZI iliyopo Mbezi Luisi na ilizinduliwa na Raisi wa VICOBA nchini Bi Devotha Likokola ambaye ndiye Mwasisi na mwanzilishi wa vikoba Tanzania.
kikundi hicho ambacho kilitimiza mwaka mmoja hapo jana kina zaidi ya Tsh 84,000,000 ambazo hukopeshana wao wenyewe kama wanakikundi. Na jana zilipatikana zaidi ya mil 3 katika harambee ya uboreshaji wa ofisi hiyo
Mwadawa akiwa na rais wa vikoba Bi Devotha Likokola ndani ya ofisi mpya ya Makazi
Raisi wa vikoba akikata utebe ikiwa na ishara ya uzinduzi wa ofosi ya Makazi Mbezi Jijini Dar jana
Bi Devotha Likokola akiwaasa wanavicoba waliohudhuria uzinduzi huo
VICOBA abavyo vilianzishwa na mwanasiasa ambaye ni mbunge wa viti maalum bi Devotha Likokola, alianzisha kwa nia ya kuwakomboa wanawake katika hali ya kuwa tegemezi na kuwafanya kuwa wajasiriamali kwa kuwafundisha mfumo endelevu wa kutegemezana kwa kuweka akiba na kukopa. Mfumo huo ambao umewanufaisha wananchi wengi na kuwafanya kuwa wamiliki wa mamilioni ya pesa kwa kununua hisa na kuweka mfuko wa jamii ambao umewasaidia wanachama wengi kuwasomesha watoto wao na wengine kununua nyumba zao wenyewe na magari kupitia VICOBA.
Bi Lilkokola ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa ofisi ya MAKAZI aliwaasa wanavicoba wote nchini kuachana na mfumo wa kuvunja vicoba kila ifikapo mwisho wa mwaka badala yake uwe mfumo endelevu ili kujikwamua zaidi. " huwezi ukawa unapanda mti halafu kila ifikapo mwisho wa mwaka unaukata, uwachekue ili uwe mkubwa ukuzalie matunda mengi baadae" alisema bi Likokola ambaye alifananisha vicoba na mti au mtoto.
mbunge huyo alisema kuwa VICOBA ni ubia wa hiari uliosajiliwa na BRELA kwa sheria ya ubia ili kuwawezesha wananchi kuwana haki ya umiliki wa fedha na mali kwani hii ni haki ya msingi kwa kila mwananchi na ili kutekeleza haki hii kwa urahisi ni vyema kila mwananchi akajiunga na vikundi vya Vicoba.
Ikiwa lengo kuu ni kumfanya mwanakicoba kuwa na maisha bora na ya furaha, thamani ya VICOBA ni kujitambua, uaminifu,kushirikisha na uwazi ili kukujitambua kujiwezesha kijasiriamali na kifedha.
Bi Likokola aliwahakikishia wanavioba kuwa ameanzisha VICOBA APPEX ambayo ni huduma ya kibenki inayotoa mikopa mikubwa kwa vikundi vya vicoba na muda si mrefu watakuwa na benki yao ambapo alisema hakutakuwa na benki yenye huduma bora na kumilikiwa na wananchi wenyewe Tanzania kama VICOBA.
VICOBA ambayo sasa imeenea nchi nzima na nchi zingine tano na wana nia ya kwenda mbali zaidi nia ikiwa kuenea dunia nziama
Bwana Daudi Nkononki ambaye ni mwenyekititi wa kikundi cha Agape akisoma risala kwa mgani rasmi
Mwenyekiti Daudi akikabidhi risala kwa Mheshimiwa Devotha Likokola
wanavioba wakimzawadia Mbuzi Mh Likokola
Mh: akifurahia moja ya picha aliyopewa kama zawadi na wanavikoba katika uzindizi huo
mmoja wa wahudhuliaji katika uzinduzi huo akitoa ushuhuda jinsi naye alivyokuwa akidhani kuwa Bi Mwadawa ni tapeli wa pesa za watu. mzee huyo aliomba msamaha kwa bi Mwadawa na kumuahidi kujiunga na VICOBA pia aliwahimiza wazee pamoja na walemavu wengine kujiunga ili kuondokana na utegemezi na kuwa mizigo kwa ndugu na jamii kiujumla
Bwana Albet Njau Coordinator wa shirika la WAT ambalo ndilo linaloshirikiana na VICOBA kuwawezesha wanavicoba kumiliki makazi yao wenyewe. shirika hili linajishughulisha na ujenzi wa nyumba za aina yoyote hapa nchini.
No comments:
Post a Comment