Thursday, October 16, 2014
MCHUNGAJI AMTOROSHA MKE WA MTU AMBAYE NI MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI
Mwimbaji
wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema anayedaiwa
kutoroshwa na mchungaji huyo. Kwa mujibu wa chanzo makini, mchungaji
huyo alifika nyumbani kwa Jonas Mrema, mume wa Janet, maeneo ya
Tegeta-Nyaishozi jijini Dar na kuishi kama mtumishi wa Mungu lakini
polepole alianza mazoea tata na Janet.
“Mume alianza kuhisi mabadiliko ya mkewe kwa mtumishi huyo, lakini
nadhani aliona ni mawazo yake tu. Ndipo siku ya siku akashangaa mkewe na
mchungaji huyo wameondoka nyumbani hapo.
“Kwa sasa tangu tukio hilo litokee ni miezi kama mitatu. Mume
alihangaika sana kumtafuta mkewe hadi jana (Jumatatu iliyopita) ndipo
akampata wakiwa na mchungaji huyo kwenye nyumba moja ambako walikuwa
wakiishi pamoja,” kilisema chanzo chetu.

Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stela Joel akilizungumzia
sakata hilo. Iliidaiwa kwamba, mchungaji huyo alipopekuliwa alikutwa na
paspoti ya nchini Burundi wakati yeye ni Mkongo wa Uvira na alionekana
kuishi nchini kinyume na sheria hivyo alifunguliwa jalada la kesi kwenye
Kituo cha Polisi cha Wazo Hili, Tegeta lenye Kumbukumbu Na.
WH/RB/7040/2014- KUISHI NCHINI BILA KIBALI.
Juzi, Amani liliwasiliana na Katibu wa Chama cha Waimba Injili
Tanzania, Stela Joel ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema
tayari chama hicho kimemsimamisha uanachana Janet kwa kitendo chake
hicho cha kumtoroka mumewe wa ndoa.
“Ni kweli na Chama cha Waimba Injili Tanzania kimemsimamisha
uanachama Janet. Hatuna mzaha katika maadili,” alisema Stela.Amani
lilimpigia simu mume wa Janet, Jonas Mrema ambapo katika mazungumzo
baada ya salamu alipewa pole kwa matatizo ya mkewe, alisema asante kisha
alipoulizwa kuhusu hali ilivyo aliomba apige simu yeye baadaye kwa vile
alikuwa kikaoni.
Hata hivyo, baada ya saa mbili kupita bila kupiga, Amani lilimpigia
tena simu ambapo iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata
zinaendelea.
Tuesday, October 14, 2014
KIJANA AKUTWA AMEFARIKI KORONGONI MKOANI KIGOMA

Mwili ukiwa bado eneo la tukio
Katika
hali ya kustajaabisha kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la
Yusuph (Me) mkazi wa Buzebazeba Ujiji amekutwa amekufa katika korongo la
Lebengera jirani na Ofisi za CCM mkoa katika manispaa ya Kigoma Ujiji
huku akiwa amejaa damu katika paji lake la uso

Mara baada ya Jeshi la Polis kufika eneo la tukio walimpekua marehemu
na kumkuta na fedha taslimu kama elfu tatu hivi na karatasi ambayo
haikujulikana mara moja imeandikwa nini


tukio hilo limetokea jana Oktoba13 eneo tajwa hapo juu huku umati
mkubwa ukiwa umefurika ili kumtambua na kushuhudia tukio hilo, katika
uchunguzi wa awali inasemekana tukio hilo limetokea jana usiku kwani
kutwa nzima ya jana hapakuonekana mtu ambae amekufa eneo,akiongea na
kibonajoro.com mmoja wa wananchi aliekuja kushuhudia tukio,na ambae ni
mfanyakazi katika ofc moja jirani na eneo la tukio jina (....) amesema
hii imekuwa ni mara ya pili kutokea tukio kama hili la mtu kukutwa
ameuwawa na kutupwa katika korongo hili,hivyo tunaviomba vyombo vya
usalama kuweka doria ya mara kwa mara eneo hili kwani eneo hili
linakaribiana na Bar pamoja na Ofisi za Hazina Ndogo.

Polisi wakichukua vielelezo katika picha

Kutokana na eneo alilokutwa marehemu kuwa na miundombinu mibovu ya
kumtoa walilazimika kutumia ngazi,hivyo waliomba msaaada wa ngazi kwa
gali la emegency la Tanesco na hapa ngazi ilikuwa inashushwa tayari
mwili kupandishwa juu kupelekwa eneo husika,


Mwili ukitolewa tayari kupelekwa kwenye gari la Polisi




Mwili ukiingizwa kwenye gali la Polis kuelekea Central Polis kwa taratibu zingine

Mwili wa kijana Yusuph ukiwa ndani ya gari la Polisi,katika taarifa
zingine zilizopotikana eneo la tukio zinasema kabla ya kugundulika kwa
tukio hili kumetokea tukio lingine linalofanana na hili maeneo ya
mwasenga usiku wa kuamkia leo mtu kukutwa ametupwa huku akiwa amepoteza
maisha.



Polisi wakiondoka eneo la tukio

kwambali ndio eneo la ofisi za CCM mkoa ambapo kulia ndiko kumetokea tukio hili.
WAZIRI LAZARO NYALANDU AZUNGUMZIA TETESI ZA KUTANUA NA AUNT EZEKIEL NCHINI MAREKANI

Aunt Ezekiel
PROFESA MAZRUI AFARIKI DUNIA
Profesa Ali Mazrui enzi za uhai wake.
MSOMI
mashuhuri wa masuala ya kisiasa, utamaduni wa Kiafrika na dini ya
kiisilamu wa nchini Kenya, Profesa Ali Mazrui ameaga dunia leo akiwa
Marekani.
Mazrui alyekuwa anaishi nchini Marekani, amefariki akiwa na umri wa miaka 81baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa zinadai kuwa Profesa Mazrui atazikwa mjini Mombasa, Pwani ya Kenya alikozaliwa.
Enzi za
uhai wake, marehemu alitoa ombi la kutaka kuzikwa Mombasa akisema
angependa kuzikwa katika jumba la kihistoria la Fort Jesus.
Kabla ya kifo chake, Marehemu Mazrui alikuwa anafundisha katika Chuo Kikuu cha Binghamton mjini New York, Marekani.
PAPAA MSOFE NA MAKONGORO WAENDELEA KUSOTA RUMANDE
Papaa Msofe (katikati) akishuka ngazi za Mahakama ya Kisutu. (Picha na maktaba yetu).
MFANYABIASHARA
anayekabiliwa na kesi ya mauaji, Marijan Abubakar, maarufu kama Papa
Msofe na mwenzake, Makongoro Joseph, wameendelea kusota rumande kutokana
na kile kinachoelezwa kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Kesi
ya watuhumiwa hao wawili imetajwa leo na mwendesha mashitaka wa
serikali, Bi Hellen Moshi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Liwa.
Msofe na Makongoro wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya bwana Onesphory Kitoli.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Oktaba 27, mwaka huu itakapotajwa tena.
KILIMO BORA CHA MANANASI KIMEBADIRI MAISHA YA WANAWAKE WA KIWANGWA NA FUKAYOSI WILAYANI BAGAMOYO.
Japokuwa
kumekuwa na dhana ya kwamba mkulima ni mtu maskini na asiyeweza kufanya
shughuli nyingine ya maendeleo, lakini kwao UFUMAKIFU wanajiuliza walikuwa wapi
kufanya kilimo hiki tangu siku nyingi.
Akiongea
na mwandishi wa habari Bi Farida Mrisho Pyara, mwenyekiti wa kikundi cha
UFUMAKIFU (Umoja wa wanawake Kiwangwa na Fukayosi) alisema kuwa kilimo cha
mananasi kimekuwa mkombozi kwao kwani tangu walipoanza kujishughulisha na
kilimo hicho kama kikudi maisha ya wanakikundi wengi yamebadirika kutoka katika
hali duni na kuwa bora zaidi.
Kikundi
hicho kilianzishwa mwaka 2012 na shirika la DotAfrika kwa madhumuni ya
kuwakwamua wanawake kimaendeleo katika kazi zao, kina wanawake zaidi ya 50 wa
umri tofauti tofauti. Walianza kwa kuwa na shamba la pamoja ambalo walilima
wanachama wote kwa kupanda mbegu mpya kutoka chuo cha SUA ambazo walipewa na
shirika hilo kama msaada.
Hata hivyo mwenyekiti huyo alidai kuwa baada ya kulima kama kikundi lakini lilikuwa ni darasa tosha kwao kwani walijifunza mambo mengi mapya ya jinsi ya kulima kilimo bora na kutumia mbegu bora za mananasi kwa kupata mavuno bora kwa manufaa zaidi.
Bi farida alisema shamba hilo ambalo lilikuwa kama ni shamba darasa kwao liliwapa mafunzo ambayo kwa sasa kila mwanakikundi ana shamba lake na analima kwa kutumia ujuzi uleule walioupata hapo awali na kila mmoja amefunguka na kutambua kuwa walikuwa wanadharau kilimo kwa kuwa walikosa elimu ya kutosha, ni jinsi gani wanaweza kufanya kilimo chenye manufaa kwao.
“Wanawake
wengi tulikuwa tunafanya biashara ndogo ndogo huku tukiwaachia wanaume kwenda
mashambani peke yao, matokeo yake wengi wetu tulibaki kuwa tegemezi na inakuwa
hali mbaya zaidi ikitokea mwanaume kafariki. Lakini tangu tumeanza kikundi hiki
wengi wetu tuna mashamba yetu binafsi ambayo hutupatia kipato cha kutosha”
alisema Bi Farida.
Hata hivyo
alisema mpaka sasa kila mwanachama anashamba lake ambalo analilima mwenyewe
kama shamba darasa, na iwapo wanapata
tatizo linalohitaji ufumbuzi wanae Afisa kilimo Bwana Amir Abdul ambaye
amekuwa msaada mkubwa sana kwao kwani ndiye anayewapa elimu ya kilimo kila
wanapohitaji elimu hiyo.
Nae Bi Halima Muhamed Athumani (58) mjumbe wa UFUMAKIFU alisema elimu waliyopewa ni bora na isiyo ya gharama katika kufanikisha kilimo hicho.
“Tumeletewa
mbegu za mananasi isiyokuwa na magonjwa yaliyokuwa yanatusumbua kipindi cha
nyumaa, na tumejifunza njia ya kulima bila kulichosha shamba wakati huo huo
tunazuia matunda yasiharibiwe na jua kwa kupanda mazao mawili shambani yaani
mananasi na migomba pamoja, wakati huo huo tunarutubisha shamba kwa kuchoma
masalia ya nanasi shambani baada ya kuvuna kitu ambacho tulikuwa hatukijui hapo awali”. Alisema Bi
Halima
“Siku hizi
huwa tunaweka mbolea ya DAP na UREA kwa ajili ya kukuzia na hatutumii dawa ya
aina yoyote kuzuia magonjwa kwani mbegu hii haina usumbufu huo. Na pia mbegu
hii inawahi kukomaa.”
Aliendelea
kwa kusema mbegu hii ni nzuri kwa kuwa hainyauki tunda wala kuozea shambani na
inatoa mazalia bora pia ambayo huwa yanakuwa ni mbeyu kwa ajili ya kupatwa
msimu mwingine nah ii ni tofauti na mbegu tulizokuwa nazo siku za nyuma
Kikundi hicho ambacho kwa sasa kimeamua kulima kilimo cha kisasa kwa ajili ya kuondoa umaskini majumbani mwao, wameamua kwenda mbali zaidi kwa kufanya biashara ya mananasi nje ya nchi na mikoa ya mbali kwa kuyasindika mananasi na kuyasafirisha.
Kikundi hicho ambacho kwa sasa kimeamua kulima kilimo cha kisasa kwa ajili ya kuondoa umaskini majumbani mwao, wameamua kwenda mbali zaidi kwa kufanya biashara ya mananasi nje ya nchi na mikoa ya mbali kwa kuyasindika mananasi na kuyasafirisha.
“Hivi
saasa tumejenga makaushio (dryer) kwa ajili ya kukausha mananasi na kuyahifadhi
vizuri kwenye mifuko tayari kwa kuyapeleka sokoni ili kuwa na tija zaidi.
alisema Mwenyekiti huyo
Kilimo cha nanasi kinastawi zaidi
katika ukanda wa nchi za joto na kwenye udongo usituamisha maji. Hapa Tanzania
zao hili linastawi sehemu nyingi lakini kwa wingi linastawi mikoa ya Pwani,
Morogoro, Shinyanga Tanga Mtwara Lindi na Bukoba. Katika mkoa wa pwani, zao
hili linalimwa katika wilaya ya Bagamoyo, Mkuranga Kibaha na Kisarawe. Kwa
Bagamoyo linalimwa zaidi katika kata ya Kiwangwa na maeneo ya Gongo.
Zao hili lina kiasi kikubwa cha
vitamini A na B na kiasi kidogo cha vitamini C, pia kuna
madini kama potasiam, kalsiam, chuma na magnesiam
Nanasi
huliwa baada ya kumenywa ganda la nje na pia hukamuliwa maji yake
na kunywa kama juisi.Nanasi pia linaweza kuanikwa na kukaushwa ambapo huliwa kwa
kutafunwa. Nanasi pia baada ya kukauka husagwa na unga wake hutumika
kutengeneza juisi au kuchanganywa katika vilaji vingine kama vile Pizza nk
Subscribe to:
Posts (Atom)














