Wednesday, August 13, 2014

KIBAKA AUWAWA KWA KUCHOMWA MOTO

 

Kijana ambaye jina lake na sehemu anayoishi haikufahamika mara moja ameuwawa kikatili kwa kuchomwa na moto na wananchi wenye hasira akidaiwa kuiba pikipiki maeneo ya katikati ya mji wa Morogoro.     
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema pikipiki zaidi ya 20 zilikuwa zimeongozana na mojawapo ikiwa imembeba kijana huyo akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi huku nyingine ikiwa imebeba dumu la mafuta na kiroba cha majani makavu. "walipofika hapa walimlazimisha ashuke huku wakimpiga na aliposhuka walimuwashia moto juu yake mpaka waloporidhika ya kuwa kafa ndipo walipowasha pikipiki zao kwa mbwembwe na kuondoka"
mmoja wa mabodaboda haoalisema kuwa kibaka huyo walimkamata akitaka kupora pikipiki kwa bodaboda mwenzao ndipo walipo mtia mikononi na waliamua kumfanyia hivyo kwa kuwa wakipelekwa polisi wanaachiwa kwa dhamana na kuendeleza uhalifu wao mtaani hivyo waliamua kufana hivyo kama fundisho kwa vibaka wengine waache tabia mbaya



Baadhi ya mashuhuda wakitazama mwili wa kibaka aliyeuawa kwa kuchomwa moto baada ya kukutwa akipora pikipiki

No comments:

Post a Comment