Wednesday, August 13, 2014

KIBONDE NA GADNER WAPANDISHWA KIZIMBANI

Watangazaji Ephraim Kibonde (wa kwanza kushoto) na mwenzake Gardner Habash (wa pili kulia) wakielekea kizimbani.
Watangazaji hao wakiongozwa na maofisa wa polisi kuelekea mahakamani.
...Wakiingia mahakamani.
MTANGAZAJI wa Clouds FM, Ephraim Kibonde na mwenzake, Gardner Habash wa Times FM leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kudharau amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi.
Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta Wambura.
Kibonde na Gadna wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.
Kesi yao imeahirishwa mpaka Septemba 10 mwaka huu itakaposikilizwa tena.(Picha na Shakoor Jongo / GPL)

No comments:

Post a Comment