Ndoa
ya mwanamuziki Judith Wambura maarufu Lady Jaydee na mtangazaji mashuhuri wa radio Gardner G. Habash
inasemekana imevunjika huku Gardner akihama Kimara alikokuwa akiishi na
mkewe na kuhamia kwa mmoja wa ndugu zake wa karibu sana.
Chanzo
cha kuvunjika ndoa hiyo bado hakijajulikana moja moja kwa moja ila
wawili hao wamekuwa katika migogoro kwa muda sasa. Hii inaeelezwa kwamba siyo mara ya kwanza
kutengana, lakini safari hii mambo yanaonekana kuwa magumu zaidi.
Katika ukurasa wake wa Instgram, Jaydee ameandika: "Walking Away From Troubles" ambapo uchunguzi unaonyesha kwamba mambo si sawa hata kidogo.
Gardner kabla ya kumuoa Jide alikuwa tayari na mke halali wa ndoa na mtoto mmoja.
No comments:
Post a Comment