Familia
inayoundwa na wanandoa Bianca na Nick Bowser, ni familia yenye furaha
lakini iliyowashangaza wengi baada ya Nick ( baba wa familia) kupata
ujauzito na kujifungua.
Iko
hivi; Nick ambaye ana umri wa miaka 27 hivi sasa, alizaliwa na jinsia
ya kike na kupewa jina la Nicole na wazazi wake, lakini aliamua
kubadilika na kuishi kama mwanaume (transgender/jike dume) tangu miaka
saba iliyopita. Na hii ilichangiwa pia na sura na umbo la kiume
alilokuwa nalo.
Hali
ilikuwa hivyo pia kwa Bianca ambaye ana umri wa miaka 32 hivi sasa,
yeye alizaliwa mwanaume na kuitwa jina la Jason, lakini kutokana na kuwa
na sura nzuri na umbo la kike, na hisia zake za kutaka kuishi kama
mwanamke, alibadili aina ya maisha na kuishi kama mwanamke kamili.
Wawili
hao walikutana na kuamua kufunga ndoa huku wakiyabadilisha kabisa
maisha ya wana ndoa, Nick akiwa baba wa familia anaevaa na kuishi kama
mwanaume. Mkewe Bianca (ambaye ni mwanaume) yeye alibadili na kuishi
kama mwanamke kamili akiihudumia familia yake na kuvaa mavazi ya kike
kama mama siku zote.
Lakini
kwa mujibu wa Bianca, wawili hao wamekuwa wakishiriki tendo la ndoa
kama kawaida kwa kuwa wanaamini kubadili kwao mfumo wa maisha hakuwezi
kubadili viungo vyao vya mwili. Matokeo yake, baba alipata ujauzito na
kujifungua. Na hivi sasa wana watoto wawili.
Cha
kushangaza ni kwamba wana ndoa hao hawawachanganyi majirani tu, lakini
pia wamewaficha hadi watoto wao wadogo ambao wanaamini kabisa kuwa
Bianca ndiye aliyewazaa na baba yao ni Nick. Lakini siri hii itakaa hadi
lini ili hali majirani wanajua na wa wanandoa hao wameshaeleza kwenye
vyombo vya habari?
Alisema Bianca.
Biana
aliendelea kujitetea kuwa kuwa jike dume/ dume jike haielezi jinsi
ulivyo. Ni kama kuwa na rangi nyeupe, nyeusi, mnene au mwembamba
haielezi kitu kuhusu jinsi ulivyo.
Kwa
upande wa Nick, anasema mara ya kwanza alipopata ujauzito wa Kai
alibadilika na kuishi kama mwanamke, hivyo ikawa kama yeye na mumewe
wote ni wanawake. Wengi walidhani wanacheza mchezo wa kusagana.
Lakini
alipopata ujauzito wa pili ndipo alipoamua kuishi maisha yake ya
kawaida kama baba na kitumbo chake. Hali ilimnyima raha mbele za watu
waliokuwa wanamshangaa sana.
No comments:
Post a Comment