Wakizunguza kwa masikitiko makubwa na
yetu lungwe blog wananchi hao wamesema
hatua hiyo imekuja kufuatia
vijana hao kuiba mahindi na vyombo vya
shule ambavyo kwa juhudi zao wali jichangisha kwa madhumuni
ya kuwawekea watoto wao
hazina ya chakula ambacho kilikuwa kinatumiwa wakati wamchana
pindi wakiwa njaa
Hata hivyo
taaarifa za awari kutoka kwa wananchi hao zilieleza kuwa
katika siku za hivi karibuni uongozi wa shule hiyo uliitisha kikao maalmu
kilicho jumuisha wazazi na
walezi ambapo kupitia kikao
hicho waliafikiana kuchangia
mahindi kilo tano kwa kila mmoja
ambazo zilitolewa na kufanikiwa kununua
masufuria manne kwa
ajili ya kuwapikia chakula watoto
wao pindi wakiwa shule.
Walisema
walishangaa baada ya
vijana hao kujichukulia uamzi
mgumu wa kubomoa ofisi ya shule na
nyumba ya mkuu wa shule kwa kutokomea na vitu hivyo
ambavyo waliweza kuvikamata baada
ya msako mkali kupita kijijini hapo.
mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, fred ngiluke mwandimila alisema vijana hao walibomoa mlango na kufanikiwa kuiba gunia mbili za mahindi na masufulia manne ya kupikia chakula na kwamba kutokana na hali hiyo kutokea waliamua kutoa taarifa katika uongozi wa kijiji ambao ulifika na kuwakamata mapema
Afisa mtenda wa kata hiyo Huluma
mwakyusa alikili kutokea kwa tukio hilo
na kwamba watuhumiwa wamepelekwa katika
hospitali ya wilaya
ya Rungwe yaani makandana na huku
wakiwa chini ya ulinzi wa
jeshi la polisi na kuwataja watuhumiwa
hao kuwa ni Sauli
mwakyage miaka {30} na tumaini mwasimbega mika {35}wote wakiwa ni wakazi wa kijiji hicho.
Kwa upande wa
walimu wa shule hiyo akiwamo
Elieza anangisye walisema kutokana
na hali hiyo imepelekea
wanafunzi wao kushindwa
kupata chakula kwa wakati
na ukilinganisha kuwa vyakula
vyote huwa vinatolewa na wazazi na walezi Ikiwa ni pamoja na wanafunzi
kushindwa kwenda shule kutokana
na msako wa vyakula kuchukua nafasi yake..
No comments:
Post a Comment