Monday, September 15, 2014

RUNGWE UCHUMI WAKE UMEJIFICHA HAPA

IMEELEZWA kuwa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imeshindwa kupaa kiuchumi kutokana na kushindwa kutumia fursa ya kuvitangaza vivutio vilivyopo ambavyo havipatikani duniani kote vitakavyopelekea wilaya hiyo ipae kiuchumi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na katibu mkuu wa Christian and Gospel Ministry (CGM)wilayani humo Watson Pamesa wakati wa makabidhiano ya jengo la kufungia mitambo kwa ajili ya matumizi ya Redio Rungwe inayotarajiwa kufunguliwa siku za hivi karibuni.

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=1486f81ed9967800&attid=0.1&disp=inline&realattid=f_i010jhi70&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-Wt9hgn5KzbaKh0D4jXCix&sadet=1410781737480&sads=oFsSPQUgvHJmIU-xa2y5Vy_djRc
Makabidhiano hayo ya jengo la ngazi moja yalifanyika jana baada ya uongozi wa Christian kuketi na wakuu wa idara kwenye ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Veronika Kessy ambapo mapendekezo na muhtasari wa kikao hicho yatapelekwa kwenye kikao cha baraza la madiwani Agosti 26 mwaka huu kujadiliwa.

Pamesa alisema waliiandikia halmashauri hiyo barua ya kutaka kukodi jengo kwa matumizi hayo yenye kumb,RDC/E.1/117/97 ya tare,07/8/2013 ambapo ilijibiwa na kusainiwa na kaim mkurugenzi wa halmashauri hiyo Elias Sangi kwa barua yenye kumb,TKY/7.6/VOL.010/2014 ya Tar,30/05/2014 kuwa ombi lao limekubaliwa.

Alisema baada ya makubariano hayo siku ya alhamisi ya tare,11/9/2014 walienda kuoneshwa jengo pamoja na mapendekezo ya ulipaji na kuwa kinachosubiriwa ni maamuzi ya madiwani ambapo wataketi siku hiyo na kutoa maamuzi.

Alivitaja vivutio hivyo ambavyo havipatikani Duniani kote kuwa ni Vinyonga na  Nyani wekundu waliopo mlima Rungwe,daraja la mungu,ziwa ngozi na kisiba wenye ambayo maji yake hayajai wala hayakauki,mti Rungwe ambao jina la wilaya limetokana na mti huo na unatibu magonjwa zaidi ya 45.

Alisema ujio wa redio hiyo utavitangaza vivutio hivyo na kupelekea watalii kuzuru wilaya hiyo na kujionea maajabu ambayo hayapatikani Duniani kote na kuwa wilaya hiyo itakuwa haishikiki kiuchumi kuliko ilivyo sasa ambapo ni ya pili kutoka mwisho kiuchumi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Christian and Gospel Ministry wilayani humo Amoni Mwakilomo mbali na kuipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa kuwaunga mkono pia amesema mchakato wa redio umefikia ukingoni na sasa wanajipanga kuanzisha gazeti kwa lengo la kutoa huduma ya kihabari kwa wanarungwe.

Chrispin Meela mkuu wa wilaya hiyo alisema watakuwa bega kwa bega na mtandao huo ili kuhakikisha wilaya hiyo inatumia Digital na kuondokana na analojia kwa kuuhabarisha umma kwa matukio mbalimbali na kukuza pato la ndani nje wilayani humo.

No comments:

Post a Comment