Monday, September 15, 2014

KIJANA ALIYEKUFA KATIKA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA SHINYANGA AFANYIWA UCHUNGUZI NA MADAKTARI



Mwili wa marehemu Musa Shija mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa mtaa wa Mwalugoye kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga aliyeuawa kwa kushambuliwa akiwa kwenye Fiesta usiku wa kuamkia JANA katika uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema uchunguzi wa kitaalam walioufanya unaonesha kuwa kijana huyo alipigwa na kitu butu kichwani na kusababisha kuvuja damu kichwani kutokana na kuvunjika kwa fuvu la kichwa.

No comments:

Post a Comment