MEYA wa Ilala, Jerry Silaa amemuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Ernest
Mangu kutokubali askari wake kuwa wakala wa sheria za barabara.
Silaa alisema hayo katika uchaguzi wa Naibu Meya uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema askari wengi wanajichukulia sheria mkononi kwa kuwakamata
baadhi ya madereva kwa madai kuwa magari yao yamezidi viwango hivyo
yanaharibu barabara pasipo kuzingatia sheria.
Pia Silaa ameitaka Mahakama ya Jiji kuacha kuwakamata wananchi kwa
makosa yasiyofaa na ambayo hayana uhakika, kuwatoza faini zisizo na
msingi na kuwaweka mahabusu bila hatia.
“Ninapigiwa simu na kupewa malalamiko mara kadhaa wananchi wanaonewa
bila sababu za msingi na kuwafanya wajione sawa na wakimbizi katika nchi
hii,” alisema Silaa.
Pamoja na hayo alisaini mkopo wa sh bilioni 1.2 kutoka Benki ya
Uwekezaji Tanzania (TIB) kwa ajili ya kununua magreda mawili ya
kutengeneza miundombinu ya halmashauri.
No comments:
Post a Comment