Mahakama
nchini Mexico imewafunga jela miaka 30 kila mmoja ndugu wa familia moja
kwa kosa la kushirikiana kumtoa macho kwa kutumia kijiko mtoto wao
mwenye umri wa miaka mitano baada ya kukataa kumuabudu shetani.Mtoto
huyo aliyetajwa kwa jina la Fernando Caleb Alavarado Rios aliamrishwa
kufumba macho mbele ya mama yake mzazi, mama yake mdogo, babu yake na
wajomba zake wakati ambapo walikuwa wanamuomba shetani ajitokeze ili
awasaidie kuepukana na janga la tetemeko la ardhi!
Lakini
kijana huyo alikuwa anaogopa kwa jinsi utaratibu wa ibada hiyo ya
kishetani iliyovyokuwa inaendeshwa hivyo akakataa kabisa kufanya hivyo.
Katika hali isiyo ya kawaida, mama yake mzazi aliyetajwa kwa jina la
Maria del Carmen Garcia Rios alimkamata kwa nguvu na kuwataka wenzake
wamsaidie kumtoa macho. Mama yake mdogo alishirikiana na mama yake na
wakatekeleza kitendo hicho cha kinyama.
Mama yake Fernando
Kwa mujibu wa UK Daily Mail watu hao walikamatwa baada ya jirani yao
kusikia makelele na kujaribu kufanya uchunguzi kujua kinachoendelea.
“Tuliweza kusikia makele na tulikuwa tunapiga hodi kwa nguvu kwenye
mlango wao lakini hakuna mtu aliyetujibu, baadae polisi wa patrol
alikuwa anapita na wanawake waliokuwa na sisi walikimbia barabarani na
kumuita, walikuja polisi wengi na walitumia nguvu kuingia ndani.”
Alieleza jirani huyo aitwae Joaquin Arguello.
Polisi aliyejitambulisha mahakamani hapo kwa jina la Benet Curiet
aliyefika kwenye eneo la tukio alieleza kuwa baada ya kufika pale
alikuta damu zikiwa zimetapaka, aliwahoji watu hao na mama yake
alijitambulisha vizuri na kukiri kuwa yeye na mdogo wake ndio
waliosaidiana kumtoa macho mtoto huyo baada ya kukataa maagizo yao
wakati wa ibada ya shetani.
Jana (September 10) ilikuwa ni miaka miwili tangu lilipotokea tukio
hilo May 2012, na mahakama imewahukumu wote waliokuwa katika ibada hiyo
kifungo cha miaka 30 jela.
Mtoto Fernando hivi sasa hana uwezo wa kuona na madaktari wamempa miwani maalum na yuko katika uangalizi wa serikali.
Chanzo: UK Daily Mail
No comments:
Post a Comment