Thursday, September 11, 2014

MCHAKATO WA KATIBA MPYA KUSITISHWA TANZANIA


Rais Jakaya Kikwete
Kumekuwa na maoni tofauti kufuatia hatua ya kusitisha mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya nchini Tanzania.
Katika kikao cha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na Viongozi wa vyama vya siasa nchini humo wamekubaliana kuwa kura hiyo ya maoni ambayo ilikuwa ifanyike kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 kinafanyika baada ya uchaguzi huo
Umoja wa wabunge wa kambi ya upinzani Tanzania UKAWA hivi karibuni walisusia bunge la Katiba na kutoka nje kwa kile walichodai kutekelezwa kwa baadhi ya madai ya msingi.
Akizungumza na BBC Deusi Kibamba Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba nchini Tanzania anasema hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kusitisha vikao vya bunge la katiba hata kabla ya muda uliopendekezwa wa Oktobar 4 mwaka huu.
Amesema kuwa iwapo wabunge hao wataendelea na vikao hivyo wao pamoja na baadhi ya wananchi wanatarajia kufanya maandamano hadi mjini Dodoma na kufunga milango ya ukumbi wa bunge.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii Robert Mkosamali anasema pamoja na kwamba fedha nyingi zimekwisha tumika hadi sasa kinachpaswa kuangaliwa si gharama hizo bali ni kuangalia ubora wa katiba inayotafutwa hata kama yaweza kutafutwa kwa muda mrefu na wka gharama kubwa.
Mkosamali amesema hata nchi zilizopata Katiba zilichukua muda mrefu na gharama kubwa akitolea mfano nchi ya Kenya.

No comments:

Post a Comment