SIKU moja kupita baada ya Rais Jakaya Kikwete kufikia Maazimio na Umoja
wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA kulisitisha bunge Maalum la katiba
na kupisha Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 ili kutoa mwanya wa kuifanyia
marekebisho ya 15 ya katiba iliyopo ya Mwaka 1977,
Nao Umoja huo wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA umeibuka na
kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka asitishe Bunge hilo mara moja na
kuacha mpango wake wa kulisitisha Bunge hilo Octoba 4,kwani kufanya
hivyo ni kupoteza pesa za Watanzania bure kutokana Vikao hivyo
vinavyoendelea haviwezi kuleta katiba bali vinaendelea kuteketeza pesa
za Wananchi,
Hayo yamesemwa leo jijini Dar Es Salaam na Viongozi mbalimbali wa
kisiasa wanaunda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA,wakati wa
Mkutano na Waandishi Habari, mkutano huo wenye Lengo la kujadili
maazimio kati ya viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),na Rais Jakaya kikwete uliomalizika Juzi Ikulu ndogo mjini Dodoma.
Ambapo naye katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Mandeleo
Chadema Dk Wilbroad Slaa amesema anamshangaa sana Rais Jakaya Kikwete
kwa kutokuwa na huruma kwa watanzania kwa kuzidi kuliruhusu Bunge hilo
kuendelea hadi Oktoba 4 mwaka
huu, kwani huko ni kupoteza pesa za watanzania kutokana na yeye Rais
Kikwete wakati wa mkutano na Vyama vya hivyo vya Kisiasa alikibuliana
nao kwamba Mwenendo wa Bunge hilo hauwezi kuleta Katiba Mpya,
“Mimi namshangaa jinsi Rais Kikwete anavyokubalia pesa za Watanzania
zipotee bure kiasi hichi pasipo kuwa na Sababu maana leo hii mpaka
octoba 4 ni siku ishirini na ukipiga hesabu za Wajumbe wote waliokuwa
Bungeni kwenye Vikao vya Bunge garama yake ya posho ni zaidi ya Bilioni
3.5 hurafu yeye mwenyewe Kikwete anakubali wazi katiba haitopatikana
sasa, huku ni kuchezea pesa za wananchi kabisa maana ukweli huko wazi
kabisa ndio maana tunamtaka sisi UKAWA alisitishe sasa bunge hilo ili
fedha hizo ziende katika mambo mengine yenye tija”alisema Dokta Slaa,
Dokta Slaa alizidi kusema anamshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa
na huruma za watanzania kwani anakubalina na watu mia sita kutoka kwenye
bunge hilo laa Bunge la katiba na kuwapuuza watanzania Zaidi ya
Milioni 40 ambao hata mlo moja kwa siku ni kazi.
“Huyo ni Rais gani huyo ambaye anashindwa hata kuwaonea huruma
watazania wanaoteseka tena hata kula mlo moja kwa siku ni kazi,yeye
anakubaliana na wajumbe mia sita kuteketeza pesa za Wananchi,hivi kweli
ndio kiongozi huyu,kwasababu kiongozi makini ni yule anayeangalia Fedha
za Chache kwa ajili ya manufaa kwa wananchi wake”alizidi kusema Dokta
Slaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha NCCR mageuzi James Mbatia
alisema wao Ukawa wamepokea kwa moyo wote maamuzi waliyofikia ya
kuifanyia marekebisho ya katiba iliyopo na kusema Bunge la katiba
litakapohalishwa basi wakubaliane kamaandishi ili Rais ajaye basi aendelee na mchakato huu asiupuuze,
“Sisi ukawa tunakubalina na kwa moyo wate maanuzi tulitofikia katika
mkutano na Rais Kikwete,na tunasema wazi tumekubaliana kuhailisha
mchakato huu basi tunataka tukubaliane kimaandishi kabisa ili Rais ajaye
baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2015 aendelee na mchakato huu atutaki kabisa
kusikia eti Rais anayekuja ahamue kwa maamuzi yake hatutati kusikia
ujinga huo”alisema Mbatia
Mbatia ambaye naye ni Mjumbe wa Bunge hilo Maalum la katiba aliongeza
kusema wao Ukawa wamefikia uamuzi kwamba endapo Bunge hilo la katiba
litakapoendelea baada ya uchaguzi mkuu hawatakubali kuongozwa na
mwenyekiti wa sasa ambaye anaongoza Samwel Sitta na kuzidi kusema
Mwenyekiti huyo hana sifa ya kuliongoza bunge hilo kutokana na
kuendesha siasa za chuki na ubaguzi.
Vilevile naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa
Ibrahimu Lipumba alisema wanamuomba Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali
kulikagua Bunge hilo la Katiba kwa madai bunge hilo lilitawaliwa na
Ufisadi wa kutisha kutokana mipango yake hiyo.
“Kiukweli namuomba Mkaguzi Mkuu wa Serika alifanyie ukaguzi wa
kimahesabu bunge hilo la katiba kutokana na Vikao vyake hivyo kutawaliwa
na ufisadi wa kutisha tumeona leo Jinsi kila mjumbe mmoja kwa siku
ametengewa bajeti ya chai ya shilingi Eflu kumi kwa siku tena chai ya
asubuhi na jioni na hata vipaza sauti pia, vyote hivi ni matokeo ya
Ufisadi ndio maana tunamtaka alifanyie ukaguzi wa kimahesabu”alisema
profesa Lipumba.
Kuhusu kama Endapo Rais Jakaya asipofanyia merekebisho katiba iliyopo?
Mwenyekiti
wa Chama cha NCCR mageuzi James Mbatia alisema endepo kama Rais Kikwete
asipofanyia marekebisho katiba iliyopo basi atakuwa amefanya usaliti
kubwa na ajue ataliweka taifa kwenye machafuko makubwa sana kwani Umoja
huo hautokubaliana na yeye.
Katika Hatua nyingene Umoja huo wa Katiba wa UKAWA umeitaka tume ya
Uchaguzi nchini ilifanyie marekebisho ya haraka Daftari la kudumu la
wapiga kura ili liweze kuwaandikisha watanzania ambao hawajapata Fursa
hiyo.
No comments:
Post a Comment