Thursday, September 11, 2014

WASAGAJI WAFUNGA NDOA BAADA YA KUISHI PAMOJA MIAKA 72


Zaidi ya miongo sabini baada ya kuanza uhusiano wa kimapenzi, Vivian Boyack na Alice "Nonie" Dubes wamefunga ndoa. Boyack, 91, na Dubes, 90, walifunga ndoa rasmi Jumamosi iliyopita, limeripoti gazeti la Quad City Times. 

"Sherehe hii ilikuwa ifanyike siku nyingi sana," amesema mchungaji Linda Hunsaker wakati akIfungisha ndoa hiyo iliyohudhuriwa na marafiki wachache na baadhi ya wanafamilia wa maharusi.

Wawili hao walikutana katika mji waliokulia wa Yale, Iowa, nchini Marekani. Baadaye walihamia mji wa Davenport mwaka 1947, Boyack akifanya kazi ya ualimu, huku Dubes akifanya shughuli za kihasibu.Dubes amesema wameishi maisha mazuri pamoja, katika miaka yote hiyo na wameweza kutembelea majimbo yote 50 ya Marekani, na ya Canada, na pia kutembelea Uingereza mara mbili.

No comments:

Post a Comment