HALI
ya Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia (CHADEMA), imeelezwa kuwa mbaya
kutokana na kushindwa kupumua kwa kutumia pua na badala yake anatumia
mdomo kitendo ambacho ni hatari.
Taarifa hiyo imetolewa jana na Kiongozi wa Operesheni Kanda ya Ziwa
Magharibi, Tungaraza Njugu, wakati Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA),
wakitoa tamko juu ya Polisi kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi
(CCM), kuhatarisha amani ya nchi.
Kiwia, alisafirishwa kwenda India usiku wa Septemba 28 mwaka huu, kwa
ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu ya afya yake kutokana na matatizo
ya mishipa ya kichwa.
Katika tukio hilo, Kiwia akiwa na mwenzake Mbunge wa Ukerewe,
Salvatori Machemli (CHADEMA), inadaiwa walitekwa na kushambuliwa na
wafuasi wa CCM Aprili Mosi 2012 usiku eneo la Ibanda Kirumba.
“Kutokana na nafasi aliyonayo ya ubunge, Serikali inagharamia jukumu
hilo na kama chama, kimechangia kufanikisha anapata matibabu na gharama
za huko ni zaidi ya dola elfu nane ambazo zitatumuika,” alisema.
Njugu, alisema vitendo vinavyofanywa na CCM vimekuwa vikihatarisha
usalama wa binadamu lakini mamlaka husika imeshindwa kuchukua hatua,
jambo ambalo ni ukiukwaji wa haki za binadamu, hivyo wananchi wanapaswa
kutambua chama hicho kimeshindwa kusimamia na kuongoza nchi.
No comments:
Post a Comment