Kenyatta amemkabidhi mamlaka kwa muda naibu wake William Ruto kwa siku mbili atakazokuwa nje. Mahakama
ya kimataifa ya ICC, inajianda kuwa mwenyeji wa mkutano maalum wa siku
mbili kuhusu kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye atakuwa rais wa
kwanza aliye mamlakani kufika mbele ya mahakama hiyo.
Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu anazodaiwa kutenda baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.Mahakama
hiyo inasama kuwa Kenyatta alihusia katika kupanga na kufadhili ghasia
za kikabila baada ya uchaguzi uliozua utata mwaka 2007/08Zaidi ya wakenya 1,000 waliuawa kwenye gasia hizo.
Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa pia kutangaza tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Kenyatta.
ICC imemtaka Kenyatta kujibu madai ya upande wa mashitaka kuwa Kenya inakataa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.
Mashahidi wa upande wa mashitaka wamejiondoa katika kesi hiyo.
Mamia ya wabunge wa Kenya wanatarajiwa kuambatana na Kenyatta kama ishara ya kumuunga mkono.CHANZO BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment