Wananchi
wa kijiji cha Ipelo
kata ya kandete wilayani rungwe mkoani mbeya wamelazika kujichangisha fedha kwa lengo la kumtafuta mganga wa kienyeji
baada ya watoto wao kufariki dunia kila
mda wa miezi {3} katika mazingra
ya kutatanisha.
Wakizungumza na kipindi hiki wakati wa maandamano ya utoaji
wa madawa katika shule
ya masingi Ipelo
wananchi hao wamesema hatua hiyo imekuja kufuatia vifo vya
ajabu kujitokeza kijiji hapo kwa watoto
wao ambao wamekuwa wakifariki kila
baada ya miezi mtatu na
wote kutokomea mahali pasipo
fahamika.baada ya mganga huyo kutoa vitu vya ajabu katika shule hiyo ambapo
alitoa utumbo wa binadamu ndani ya Rambo pamoja na moyo wa ngombe ndani ya kichupa ukiwa unahema.
Majabu.
Hata hivyo imeelezwa kuwa mpaka
sasa watoto wanne
walifariki dunia katika
mazingira ya kutatanisha
na kwamba hali hiyo
huwa inajitokeza kwa
wanafunzi wa darasa
la nne ambao mpaka sasa wamegoma kwenda shule wakiogopa vifo hivyo.
Aidha
wakazi wa kijiji hicho wameomba msaada kwa serikali na
watumishi wa mungu kwa ujumla kuwasaidia janga hilo ambalo limeonekana kuwa kelo
kwa kwao.
Sambamba na hayo ikumbukukwe
kuwa vitu
hivyo viliweza kutolewa
na mganga huyo vikiwa
vimefukiwa na mtu au watu katika ofisi ya
mkuu wa shule na
vikisadikiwa kuwa ndiyo chanzo
cha matatizo hayo.
Kwa
upande wa viongozi wa mitaa
hiyo wamesema hawawezi kuzungumza chochote juu ya suala hilo kutokana
na kwamba serikali haiamiini masuala ya
kishirikina na kwamba mganga huyo
ameitwa na wananchi husika
bila wao kushirikishwa chochote.
No comments:
Post a Comment