Sande Jacob
Mremi amefariki Siku chache baada ya kukosa usafiri wa ndege ambapo
alitakiwa kwenda nje ya nchi kupata matibabu.Kituo cha ITV kiliripoti
kuhusu habari za kijana huyo kuumwa na kutokana na kusumbuliwa tatizo la
uzito mkubwa nakushindwa kupata Ndege ya kumsafirisha kwenda kwenye
matibabu India kijana huyo amefariki Dunia.Ndugu wa kijana huyo
walilalamika kutoridhishwa na baadhi ya Mashirika ya Ndege kwa kushindwa
kuwasaidia kumsafirisha ndugu yao.Katika mahojiano na ITV mama wa mtu
huyo amesema; “..yaani kwa kweli mashirika ya Ndege hayakuweza
kutufanyia haki kwa kweli, wametunyanyasa kwa sababu tulipokuwa
tunapeleka maombi tunataka kumsafirisha mtoto wetu ilikuwa wao
watusaidie na kutupa maelekezo tunatakiwa tufanye nini na nini, lakini
baada ya kuona tunakosa msaada ndio tukaamua kuja ITV ili watusaidie,
kwa hiyo yeye mwenyewe akaanza kupata presha kwa sababu presha alikuwa
hana mpaka anapanga kusafiri alikuwa hana presha nilimpima vipimo vyote
alikuwa hana tatizo lolote…”
Dada wa
marehemu amesema; “..Ethiopia walitusaidia kwa kweli mpaka hatua ya
mwisho na Jumapili kama Mungu angemuweka hai Ethiopia wangemsafirisha,
na mashirika ya Ndege mengine yalitakiwa yatuelekeze hivi, lakini sasa
kutokana na ile hali mara leo kapelekwa kesho anarudishwa mdogo wangu
kesho kutwa kapelekwa amerudishwa mdogo wangu, msongo wa mawazo umemkaa
rohoni anashindwa kuongea maskini ya Mungu, mawazo paka yamemfanya mdogo
wangu alikuwa hana presha paka presha imekuja paka mdogo wangu
anafariki.
Baba wa
Sande amesema; “…wakatumia sheria ya pili ya kunihusisha mimi
wakaniambia bwana kumbe mtu huyu ni mkubwa sana tunatakiwa tuvunje viti
tumbebe, nikawauliza nikulipeni bei gani? wakaniambia tulipe dola elfu
saba mia tano na thelathini na nne, na mara ya kwanza tulilipa dola elfu
sita miambili ishirini…”
Bado haijafahamika kama Shirika hilo la ndege litarudisha hela ambayo ililipwa na watu hao kwa ajili ya kumsafirisha ndugu yao.
No comments:
Post a Comment