Sunday, August 24, 2014

WATUHUMIWA 7 WA MAUAJI YA ALBINO WATIWA MBARONI

JESHI la polisi mkoani Simiyu limefanikiwa kuwakamata watu saba wanaodhaniwa  kuwa wauwaji wa aliyekuwa mlemavu  wa ngozi (albino) Munghu Mugata (40) aliyeuwawa kwa kukatwa mapanga  mnamo mwezi mei  katika  kijiji cha Gasuma kata mwaubingi wilayani  bariadi.

Akiongea na waandishi wa habari ofisi kwake, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa ambaye pia ni mkuu wa mkoa Paschal Mabiti, alisema kuwa kati ya watuhumiwa hao mmoja ni mganga wa jadi.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Kudawa Yelema (52) ambaye ni mganga wa jadi, Sitta Maduhu (39), Jasamila Sungwa (42), Mpamba Saguda (18), Dede Madono (54), Majeshi Sunja (38), pamoja na Mabula Bindondo (52) wote wakulima na wakazi wa kijiji cha Gasuma

Alisema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na wasamaria wema, liliendesha msako mkubwa wa kuwasaka wahusika wa tukio hilo, ambapo lilifanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao saba.

Alibainisha kuwa Dede Madono (54) mmoja kati ya watuhumiwa hao, aliugua ugonjwa wa malaria wakati akiwa maabusu na kupelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Bariadi, ambapo alifariki dunia akiwa hospitalini hapo akipatiwa matibabu.

Mabiti alieleza  jeshi la polisi bado linaendelea kumsaka mdhamini wa mauaji hayo, pamoja na kutafuta sehemu viungo vya mlemavu huyo wapi vilipelekwa ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani na kujibu tuhuma zinazowakabili.

Aidha mkuu huyo wa mkoa alieleza kuwa marehemu Lughata alimwacha mtoto wake Tiri Kulwa (8) darasa la kwanza, ambaye alieleza kuwa kwa sasa mtoto huyo anahudumiwa na halmashauri ya Wilaya ikiwemo kumsomesha.

Hata hivyo mkuu huyo alizitaka  wilaya zote kuhakikisha wanakusanya takwimu sahihi za watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwa pamoja na kutambua mahali wanapoishi.

Alisema mbali na kuagiza kukusanywa kwa takwimu hizo viongozi ngazi ya vijiji na kata wameagizwa kuhakiksha albino wote wanawekewa ulinzi wa kutosha kwa kushirikina na wanachi katika maeneo wanakoishi.

Sambamba na hilo mabiti alitoa onyo kali kwa watu wanatenda matukio hayo na kuwataka kuacha mara moja, huku akieleza kwa atakayebainika kutenda unyama huo utakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Tukio hilo lililotokea mei 12 mwaka huu katika kijiji ca Gasuma kata ya mwaubingi Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, baada ya mlemavu  wa ngozi Mugata kuvamiwa na watu wasiojulikana majira ya saa 8 usiku  akiwa amelala nyumbani kwake.

HII NDIO MAITI ILIYOZIKWA MIAKA 700 ILIYOPITA YAKUTWA HAIJAOZA,


Maiti hiyo ikiwa imetolewa nje ya jeneza

Ama kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni....Maiti ya mwanamke iliyozikwa miaka 700 iliyopita yagunduliwa China ikiwa haijaoza. Ipo katika hali nzuri kiasi kwamba bado ina nyusi. Inasemekana alihifadhiwa vizuri na inaonyesha alikuwa ni mtu kutoka katika familia ya ufalme. 
Maiti hiyo iligunduliwa na wafanyakazi wa barabara (wakandarasi) huko China mashariki walipopewa kaziya kupanua barabara katika mji wa Taizhou, Mkoani wa Jiangsu. Wakandarasi hao walitakiwa kuchimba kwenda chini kiasi cha futi 6 ili kumaliza mwinuko uliokuwa katikati ya bara bara ndipo wakakutana kitu wasichotarajia kukikuta.
Walipokuwa wakichimba walikuta kitu kigumu  na baada ya kufanya utafiti wao kidogo ndipo waligundua kuwa kulikuwa kuna kaburi alilozikwa mtu na ndipo wakawaita wataalamu ili kuchunguza zaidi, baada ya hapo wakaamua kuweka wazi juu ya tukio hilo kuwa waligundua kwamba kaburi hilo lilikuwa na umri wa miaka 700. Tazama picha zaidi la sakata hilo hapa chini...
Mkandarasi akijaribu kuvunja zege lililozunguka sanduku lakini kabla hawajajua kuwa kuna maiti
Baada ya kuvunja sanduku hilo la zege
Wakihamaki baada ya kuona kitu ndani ya sanduku
Wakianza kufunua matambara yaliyo ndani ya sanduku yaliyozunguka maiti

FUNDI AUWA, ATUPWA BWAWANI NI BAADA YA KUPOKEA MSHAHARA WAKE



Chande Abdallah na Deogratius Mongela FUNDI ujenzi aliyefahamika kwa jina la Omari Mkulu (25) amedaiwa kuuawa na kutupwa ndani ya bwawa baada ya kudaiwa kutoweka nyumbani kwa takriban siku tatu.
Mwili wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Omari Mkulu (25)ambaye alikuwa fundi wa ujenzi.
Tukio hilo lilitokea maeneo ya Mabwawa Saba, Mabibo jijini Dar ambapo majirani wa eneo hilo walidai kuwa waliiona maiti ya Omari ikiwa inaelea kwenye moja ya bwawa eneo hilo lakini kutokana na maiti hiyo kuvimba haikuwa ikitambulika.
Mmoja wa ndugu wa marehemu Omari Mkulu akilia kwa uchungu.
Kwa mujibu wa marafiki zake ambao walifanya jitihada za kusafiri hadi Chanika kwa baba wa marehemu ili kuhakikisha kama kweli maiti ile ilikuwa ni ya Omari na kuthibitisha kuwa ni kweli, walidai kuwa kabla marehemu hajatoweka, alilipwa fedha zake za ujenzi ambapo ilidaiwa kuwa alikwenda kuzitumia kwenye pombe mpaka usiku wa manane.
 
Bwawa lililopo eneo la Mabibo (Mabwawa Saba) ambapo maiti ya marehemu Omari Mkulu ilikutwa ikielea.
“Siku ile marehemu alikuwa amelewa sana kwa sababu alikuwa amepata fedha zake za malipo, tangu siku ile hakuonekana tena mpaka leo hii. Kwa kuwa sura na mwili wake umevimba tumezitambua nguo zake alizovaa,” alisema mmoja wa marafiki hao aliyeiomba hifadhi ya jina.
Waandishi wetu walipofika katika eneo la tukio, waliishuhudia maiti hiyo ikitolewa kwenye bwawa hilo ambapo umati wa watu waliofika katika eneo hilo walipewa nafasi ya kumtambua ambapo mmoja wa watu waliofika alidai kuwa mtu huyo ni jirani yake, akawaelekeza waandishi nyumbani kwa marehemu.
 
Marehemu Omari Mkulu (kushoto) akiwa na marafiki zake enzi za uhai wake.
Waandishi wetu walifika nyumbani kwa marehemu na kuzungumza na mama mkubwa wa Omari aliyejitambulisha kwa jina la Zainabu Omari ambaye alisimulia kwa uchungu kuwa mwanaye huyo alitoweka nyumbani Agosti 10, mwaka huu baada ya kumpatia shilingi 2,000 alizomuomba.
“Siku hiyo alikuwa na shilingi 5,000 mimi akanipa shilingi 2,000 halafu akaniambia kuwa jioni ya siku hiyo kuwa akipata hela ataelekea kwa baba yake Chanika, sasa tulishangaa tu kikapita kimya hakurudi nyumbani kuaga wala kuchukua nguo zake mpaka sasa tumesikia amekutwa amefariki dunia bwawani,” alisema kwa uchungu mama huyo.
CREDIT: GPL

HII NI HATARI!!!! WAMGEUZA MTOTO MFANO WA CHAKULA

Familia ya kichina imekosolewa vikali na watu mbalimbali wanaopigania haki za watoto baada ya kuonesha picha ya mtoto wao mchanga akiwa katikati ya misosi huku akiwekewa mboga kama sehemu ya salad.
Mama yake mzazi, Qu Quan amesema kuwa wao walifanya kwa utani na walikuwa wakicheka sana kumuona mtoto akijaribu kuamka kutoka kwenye bakuli hilo huku akishindwa na kuendelea kulia na kisha wakamtoa.
Hata hivyo, sio wote waliowakosoa seriously, wengine walitania “Chinese people are capable of anything. The baby could be one of the menu.”

WATUHUMIWA WA WIZI WACHOMWA MOTO TABATA JIJINI DAR JANA


Vijana wawili wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao hawakufahamika majina yao, wanaodaiwa kuwa ni vibaka  alfajiri ya leo wameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kumpora pochi dada mmoja mkazi wa Tabata Liwiti.
 
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema baada ya vibaka hao kumpora pochi dada huyo, walitaka kutoweka na bodaboda ndipo wananchi walifanikiwa kumkamata aliyeipora pochi hiyo akaanguka chini wakaanza kumpa kipigo huku mwenzake akifanikiwa kuondoka.
 
Kama waswahili wasemavyo za mwizi arobaini, kibaka huyo aliyekuwa akiendesha bodaboda kwa kasi, hakufika mbali pikipiki yake ikapata pancha naye akakamatwa na kuanza kupewa kichapo kisha walikusanywa pamoja wakavishwa matairi na kuchomwa moto.
 
Baada ya kuteketea kwa moto, polisi walifika eneo la tukio wakachukua mabaki ya miili ya vibaka hao na kuipeleka tatika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 

WATOTO WAOKOA MAISHA YAO KWA KWENDA KWENYE KITUO MAALUMU CHA ALBINO


Watoto wenye ulemavu  wa ngozi  katika kituo maalumu cha kulea  watoto hao Buhangija Manispaa ya Shinyanga, wamezidi kuongezeka kituoni hapo  kutokana na wimbi la mauaji ya albino  kuibuka tena. 
Hadi juzi kituo hicho kilifikishiwa watoto zaidi ya  100. 
Pia  watoto wengi wametoka kwenye mikoa ya Tabora, Simiyu na Mwanza. 
Mei mwaka huu mwanamke mwenye ulemavu wa ngozi aliuawa mkoani Simiyu na wengine wawili mkoani Tabora. 
Taarifa iliyotolewa wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada iliyopatikana kupitia harambee iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali Easy Flex la mjini Shinyanga  kwa kituo hicho, imesema kwamba tangu mauaji hayo yaanze upya kila siku watoto watatu mpaka wanne wenye ulemavu wa ngozi wanapokelewa kituoni hapo. 
Aidha watoto waliopata nafasi ya kuzungumza waliiomba serikali kusimamia kidete uhai wao. 
Rehema Masunga, Mkama Shakengwa na Daniel Limbu wanaosoma darasa la saba katika Shule ya Msingi Buhangija, walisema Tanzania inasifika kwa kuwa na amani lakini sasa hali inaelekea kuwa mbaya kutokana na baadhi ya watu kuwa na roho za kikatili na kuuwa binadamu kama wanyama . 
“Inasikitisha sana kuibuka tena mauaji ya albino tuliona kwenye vyombo vya habari watu wamekatwa mkono, naiomba jamii iwapuuze waganga wa kienyeji maana ndiyo wanachangia, tumuamini Mungu atatuepusha na unyama huu wa kikatili,” alisema Limbu.
 Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ambaye pia ni msimamizi wa kituo, Peter Ajali, akizungumza kwenye hafla hiyo mbele ya Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Ghulam Hafidh aliitaka jamii kuwa na utamaduni wa kusaidia kituo hicho,badala ya kutegemea msaada kutoka kwa wafadhili huku akisisitiza mikoa yote iliyopeleka watoto kutoa michango itakayosaidia kukidhi mahitaji na kuwaomba kuielimisha jamii umuhimu wa kusaidia. 
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Easy Flex, Happiness Kihama alisema changamoto kubwa iliyopo ni uelewa mdogo kwa jamii, juu ya kusaidia vituo hivyo vyenye mahitaji maalumu wazee na walemavu kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uchakavu wa majengo, chakula na malazi.

 

MH:WAZIRI AAMUA KUVUA SUTI NA KUSAIDIA MAJERUHI,ATOA HUDUMA YA KWANZA

Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Kondakta wa Gali lililopata ajali mara baada ya Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana kuuguria maumivu makali kwenye Mkono.Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa Kondakta wakati Roli hilo likianguka na baadae kuinuka kutokana na kugonga Ukuta pembezoni mwa Barabara ya Iringa-Morogoro.Mh:Mwigulu Nchemba akitoka huduma ya Kwanza kwa Majeruhi wa ajali hiyoMh:Mwigulu Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa Majeruhi kabla  ya kumkimbiza kwenda hospitali ya WIlaya ya Mikumi.

Na.Festo Sanga.
Naibu waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu Nchemba jana alifanya jambo kubwa na lakibinadamu kwa kuamua kusitisha safari yake kwa muda akielekea Iringa iliasaidi Majeruhi wa ajali ya Roli Kubwa lililokuwa likitokea Dsm kuelekea Barabara ya Iringa.
Ajali hiyo ambayo ilitokea mbele ya Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa nyuma ya Roli hilo kabla ya Kugonga Ukuta na Kuanguka haikuleta madhara makubwa.

.Huyu ni Dreva akijaribu kuwasha Gari hilo.
 
Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni mara kadhaa amekuwa akisaidia kuokoa majeruhi kwenye ajali anapokutana nazo barabarani,hata kwenye ajali hii alilazimika kuhakikisha majeruhi wanaokolewa na kukimbizwa Hospitali kabla ya hatua kubwa zaidi za Hospitali kuendelea,Katika ajali hiyo Mh:Mwigulu Nchemba alitumia Boksi lake la Msalaba Mwekundu(First Aid Kit) kuhudumia majeruhi hao iliwasitoke sana Damu.
Wananchi na Madreva waliopata kusimama kwenye ajali hiyo,Walimpongea sana Mh:Mwigulu Nchemba kwa namna alivyosaidia kuokoa Watanzania wenzake kwenye ajali hiyo,Wengi walisikika wakiomba Viongozi wengine waige mifano hii ya Mwigulu ya Kusimama na kuhudumia wahanga wa ajali,Kwa sababu imekuwa ikitokea Viongozi wanapoona ajali hawasimami kwa madai wanawahi ratiba za kazi zao.